﹑﹑ ENDELEA KUISOMA HII STORY YA UKWELI INAELEKEA PATAMU - TopicsExpress          

﹑﹑ ENDELEA KUISOMA HII STORY YA UKWELI INAELEKEA PATAMU SANA ﹑﹑ Ilipoishia Johnson alirudi kazini saa 4 usiku akakuta anapowekaga funguo yake haipo alijiuliza maswali mengi sana aliposukuma mlango wake akakuta umefungwa kwa ndani akazidi kuchanganyikiwa alianza kugonga kwa hasira akasikia sauti ya Maria ndani inamkaribisha Endelea Johnson aliugonga ule mlango kwa nguvu akasikia sauti ya Maria ndani inamwambia bby nakuja kukufungulia Johnson akaguna ile sauti ndo ikamchanganya kabisa hakuamini kabisa kuwa Maria kaja nyumbani kwake usiku wote ule wakati siku chache tu zilizopota alilala naye kwake wazazi wake wakamletea balaa Maria alifungua mlango akamkumbatia Johnson lakini Johnson hata hakumfurahia akamsukuma akamuuliza we Maria kwanini hadi mda huu upo hapa wakati juzi tu umelala huku wazazi wako wakaja kunikamata?? Maria akamjibu mbona unapanic mpenzi wangu punguza hasira nikueleweshe kaa hapa kitandani nikuambie kwanini nimejiamini hadi nimekuja usiku wote huu huku kwako Johnson alikasirika sana Maria alivyomwambia vile akatua mzigo wake aliokuwa ameubeba akakaa kitandani amsikilize Maria anachotaka kumuambia Maria akamuambia bby usikasirike mpenzi wangu kuniona niko huku kwako hadi mda huu Baba na Mama tangu jana hawapo nyumbani wameenda kwenye msiba Morogoro pale nyumbani tumebaki mimi,housegirl pamoja na mlinzi wa getini mimi nimeshindwa kuvumilia sijaonana na wewe siku mbili nimembembeleza mlinzi nimempa pesa kaniruhusu nitoke ndo nimekuja huku kwako kwa hiyo hata usiwe na wasiwasi mpenzi wangu Johnson alimsikiliza Maria kwa makini akamuuliza we unajuaje kama wazazi wako wamempa mtu kazi ya kukufuatilia itakuwaje umempa mlinzi wenu hela housegirl wenu akibanwa akiongea kuwa wewe hujalala pale kwenu itakuwaje?? Maria akamjibu housegirl wetu hawezi kufanya kitu kama hicho bby mimi na housegirl tunaiva sana na yeye pia nimeshaongea naye Johnson kusikia yale maneno hasira zote zikamuishia akalainika akamwambia Maria lakini Maria kuwa makini sana wazazi wako wanapajua hapa kwangu saivi wanaweza wakarudi mda wowote wakakuta wewe haupo wakija huku wakikukuta sijui itakuwaje Maria akamwambia usiwe na wasiwasi mpenzi wangu wanavyorudi najua lazima wapige simu nyumbani mimi nimempigia mama simu leo kaniambia wanarudi kesho kutwa Kusikia vile kidogo wasiwasi wa Johnson ukapungua Maria akampashia Johnson maji ya kuoga Johnson akaoga Maria alikuwa amempikia Johnson chakula kizuri akamtengenezea na Juice Johnson alifurahia sana kile chakula alichopikiwa na mpenzi wake wakala pamoja wakapiga stori hadi mda wa kulala ulipofika Usiku ule walipeana mapenzi motomoto kama ndo mara ya kwanza wanaonana kila mmoja alimmisi mwenzake sababu toka waanze mapenzi yao hawakuwahi kupitisha siku mbili bila hawajaonana kwa hiyo walipeana mambo mazito sana ile siku Asubuhi kama kawaida Johnson aliwahi kuamka akaanza kujiandaa kwa ajili ya kwenda gengeni kwake Akamuuliza Maria bby kwa hiyo wewe unaondoka saa ngapi?? Maria akamjibu mimi leo siendi chuo nalala hapa hadi mchana ndo naenda nyumbani kuangalia kinachoendelea Johson akamwambia mimi naondoka nakuomba uwahi kwenda kwenu wazazi wako wasije wakarudi ghafla wakute haupo Inaendelea GONGA LIKE KAMA UNAPENDA STORY IENDELEE
Posted on: Sun, 20 Oct 2013 08:51:57 +0000

Trending TopicsRecently Viewed Topics
© 2015