Habari za asubuhi marafiki zangu wapendwa.Namshukuru sana Mungu - TopicsExpress



          

Habari za asubuhi marafiki zangu wapendwa.Namshukuru sana Mungu kwa ajili ya siku hii ya leo,ambapo nina sheherekea siku yangu ya kuzaliwa.Shukrani nyingi ziende kwa wazazi wangu wapendwa Mzee wangu Mgonja ambaye licha ya kuwa ni miaka mitano sasa siko naye lakini mawazo yake,misimamo yake na upendo wake kwa familia yake vimekuwa nguzo kubwa kwangu na familia kwa ujumla eee mwenyezi Mungu akurehemu huko uliko! LOVE YOU DADDY.Namshukuru sana mama yangu mpendwa ambaye amenileta katika ulimwengu huu, amesimama kwa ajili yangu kila nilipo kuwa na shida.Amekuwa baba yetu, mama yetu na dada yetu mimi na wadogo zangu nakupenda sana mama yangu Mungu aendelee kukulinda kwa ajili yetu wanao,pia niwashukuru wadogo zangu wote kwa utulivu wao katika kipindi kigumu tulichopitia keep it up boys.Mwisho ni kwenu ninyi marafiki zangu ambao mmekuwa nami kila wakati iwe Singida,Iringa au chuoni UDSM nawapenda wote Mungu awape maisha marefu.Tusome wote Zaburi ya 23.Siku njema kwa wote."SISI SOTE KWA PAMOJA WE SHALL OVER COME"
Posted on: Thu, 15 Aug 2013 07:08:32 +0000

Recently Viewed Topics




© 2015