KWA MA-PRODUCER na WADAU wa MUZIKI... Kwa ubora wa kazi zenu - TopicsExpress



          

KWA MA-PRODUCER na WADAU wa MUZIKI... Kwa ubora wa kazi zenu inapaswa moja kwa moja tuwatambue.... Wewe ni Producer na ili tukutambue cha Msingi hakikisha Unanyonga Biti Kali, Ingiza Vocal Poa, Fanya Mixing ya Ukweli na Ukiweza fanya pia na Mastering, hakika hapo utatambulika tu watake wasitake. Ubora wa kazi zako na kwa style yako pekee vitakutambulisha. KWA NINI NASEMA HAYA: Naona huu mtindo wa kila Producer/Mtayarishaji wa Muziki kujitaja au kutaja Recording Lebo kwenye nyimbo anazo-produce umeenea na kuwa fasheni kwa muziki wa hapa bongo. Binafsi nadhani sio mbaya kwa Msanii ndani ya ngoma yake iwe kwenye Intro, Outro au kwenye Mistari yake kumtaja Producer au Recording Lebo...... "Unaonaje MAJANI". Nawapongeza kwa jitihada zenu kwa kuweza kuufikisha Muziki wetu hapa ulipo na naelewa labda inaweza kuwa ni "MTINDO MPYA" na sio kitu kibaya ila najaribu tu kushauri, kwani mbona kina Dr. Dre tunawaelewa...? Mwezi Mpya Mwema..! DC....
Posted on: Thu, 01 Aug 2013 06:23:15 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015