KWA WAPENZI WA KABUMBU TU Klabu ya barcelona imekubali kumuuza - TopicsExpress



          

KWA WAPENZI WA KABUMBU TU Klabu ya barcelona imekubali kumuuza mshambulizi wake David Villa kwenda atletico madrid kwa dau la £5milion pungufu ya £7m ambazo arsenal na spurs walifika. Hii ni kwamba walimu wengi wa mchezo wa mpira barani ulaya wamekuwa na mbinu mbadala ya kutokubali kuuza wachezaji nyota kwenda kwenye timu ambayo wanajua watakuwa nayo kwenye michuano ya ulaya. Villa anaenda Atletico madrid,hana watu wanguvu wa kuweza kuleta ushindani mbele ya barcelona au real madrid.lakini angekuwa kati ya Arsenal au Spurs angekutana wengine walio vizuri na kutishia ustawi wa barcelona. Hili si kwa barcelona tu,REAL MADRID na GONZALO HIGUAIN kwenda Arsenal,MANCHESTER UNITED na hadith ya WAYNE ROONEY na LUIS NANI. Unaona timu kama Monaco inauziwa wachezaji wa kiwango cha juu coz haichezi michuano mikubwa ya ulaya hivyo kutokuwa na madhara kwa vigogo hivyo.ikifikia wakati wakawa kama PSG hawataweza kuuziwa wachezaji kama sasa. HUU NI MCHEZO MWINGINE MCHAFU KTK SOKA COZ UNAUA USHINDANI WA KWELI. ni mtazamo wangu tu.
Posted on: Mon, 08 Jul 2013 17:07:03 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015