RIWAYA :NANI ANIFUTE MACHOZI? MTUNZI :CHARLES J LIGONJA SEHEMU - TopicsExpress



          

RIWAYA :NANI ANIFUTE MACHOZI? MTUNZI :CHARLES J LIGONJA SEHEMU YA MWISHO. 0714 79 77 78 Haikuwa rahisi kwa Frank kuendelea kusubiri kumuona mke wake,alitaka kumuona haraka ili ajue anaendeleaje na sio yeye tu bali hata mtoto wake mchanga anaendeleaje kwani siku hiyo wanapata ajali walikuwa wote. ‘Sitaki kuendelea kuwepo hapa bila kujua maendeleo ya mke wangu’ Alisisitiza na kutokana na cheo chake na heshima basi hakukuwa na namna zaidi ya kumruhusu akamuone mke wake.Aliongozwa kwenye chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu zaidi intensive care unit (ICU). ‘Kwanini hamkuniambia haraka, angalia hali ya mke wangu’ ‘Samahani bosi’Clara alikuwa kwenye hali mbaya sana,mashine za kupumulia zilikuwa puani mwake,Clara alikuwa usingizi,hainui mkono wala wa kufungua macho,kila mtu alimuhurumia kwa hali aliyokuwa nayo na kibaya zaidi siku kama tatu nyuma alikuwa mzima na afya yake,mtoto wake nae alikuwa mzima mwenye afya tele. ‘Kwanini mimi lakini, huyu tena anitoke?’ ‘Hapana bosi, kuwa na subira atapona tu’ ‘Mh! ‘ Kuanzia kiunoni mpaka miguuni alikuwa kwenye bandeji,miguu ilikuwa imepondeka vibaya sana,hata akipona sio mtu wa kutembea tena,Clara atakuwa kilema na hicho ni kilema cha maisha tena cha ukubwani,iliuma sana. ‘Aliyesababisha ajali nae yuko wapi?’ ‘Yeye anaendelea vizuri, amefungwa mhogo (POP) yuko wodini’ ‘Twende’ Hakuna wa kuweka pingamizi walinuka kwa pamoja na kuelekea kwenye wodi ya wanawake,iliwachukua kama dakika kumi hivi mpaka kufika kule na baada ya kufika walisubiri kwa muda Fulani kwani madaktari walikuwa na yao ya kufanya na walipomaliza basi waliruhusiwa kumuona. ‘Pole sana Frank’ mmoja wa daktari aliyempokea Clara aliongea. ‘Asante, hakikisha unafanya kila linalowezekana kuokoa maisha ya mke wangu,tuna mtoto mdogo anaehitaji malezi ya baba na mama,tafadhali!’ ‘Tutajitahidi bwana Frank’ ‘Kazi njema’ ‘Habari yako mama’ Frank alisalimia kwa upole. ‘Usiniue Frank, nisamehe’ ‘Patricia!’ ‘Jamani kumbe mnafahamiana!’ kila mtu alipigwa na butwaa baada ya kuona wawili hao wanafahamiana. ‘Kwanini umeamua kuiangamiza familia yangu?’ ‘Nisamehe sana’ ‘Umeamua kuonekana tena kwenye maisha yangu na sasa umekuja kwa kutaka kumuondoa mke wangu, kwanini ?’ ‘Mke wako yupi tena?’ Frank alishindwa kuendelea kuongea,alishikwa na hasira kwani hakutaka tena kumuona huyo mwanamke,mwanamke aliyeharibu maisha yake na sasa kumpata mwanamke aliyefanya maisha yake yawe ya kheri nae kamtenda vingine.Frank alishindwa kuendelea kukaa mle ndani aliona dalili za kupiga na mtu na kuleta maafa,alitoka nje ya ile wodi na kuelekea kuliko na mke wake. Akiwa njiani alikuta nesi akija kwa kasi mbele yake na alipomfikia alimwambia amfuate.kwa kweli hakujua kuna nini kimetokea na hakutaka kuuliza kwani angeweza kupata mshituko ambao ungemfanya kushindwa kupanda ngazi. ‘Mk eo anakuita,kuna kitu anataka kukueleza’ ‘Amezinduka?” ‘Ndio’ ‘Sifa za pekee ziende kwa baba aliye juu’ ‘Amina’ Walipoingia kweli Clara alikuwa macho. ‘Nakupenda sana mume wangu’ ‘Nakupenda pia ‘ ‘Uliyetoka kumuona ni nani?’ ‘Aliyesababisha ajali’ ‘Anaitwa nani na anaendeleaje?’ ‘Huwezi amini mke wangu,ni Patricia’ ‘Kumbe ndoto zangu zilikuwa za kweli, nilikuwa namuona mahali Fulani akilia na kujuta, akilitaja jina lako na kutaka umsamehe kwa yote aliyokutendea’ ‘Wapi,nani amsamehe?’ ‘Najua ngumu sana lakini hakuna namna jifunze kusamehe’ ‘Nambie kwanza unajisikiaje?’ ‘Nataka mwanangu umlee vizuri na hilo ndilo hasa litanifurahisha huko niendako’ ‘Unaenda wapi, jaman mbona unanichanganya kaa name tulee mtoto wetu’ ‘Siwezi Frank, nimeitwa na baba’ Ilikuwa ngumu sana kwa Frank kuweza kuvumilia yote anayoongea mke wake lakini ukweli ulibaki pale pale kwani baada ya kuongea “naitwa na baba”alifunga macho na kukiachia kiganja cha Frank, Clara akawa baridi. ‘Clara mke wangu tafadhali usiniache, kuwa nami’Tayari Clara aliaga dunia,Frank alikuwa akiongea peke yake na baada ya kuona hajibiwi aliamua kumwita nesi. ‘Nesi mke wangu haongei,njoo tafadhali’ Nesi alifika na kumpima na baada ya muda alimwomba Frank atoke nje kitu ambacho hakikuwa rahisi hata kidogo kwani aliuliza kwanini atoke na kumuacha mke wake hana kauli na kama tatizo kubwa basi wamwambie kuliko kutaka kuficha ukweli. ‘Sitoki mpaka uniambie amekutwa na nini mke wangu?’ ‘Nataka nikamwite daktari aje ampime’ ‘Ngoja nikamwite’Frank aliinuka na kutoka na alipoinuka tu nesi alitoa simu na kumpigia daktari na kumpa taarifa ya kifo cha Clara na ujio wa Frank ofisini kwake. ‘Basi sawa nitajua namna ya kumweka sawa’ ‘Unaitwa dokta,mke wangu haongei tena’ Bila kipingamizi aliinuka na kuongozana na walipofika alimpima na kumtaka Frank amfuate ofisini,mpaka hapo Frank alipata jibu kwamba mke wake hayupo tena,aliumia sana. ‘Naua, niacheni naua’alipiga kelele na kuanza kukimbia kuelekea wodi ya wanawake alikolazwa Patricia na alipofika kule tayari walinzi walishaambia nini kimetoke hivyo walijipanga kumdhibiti. ‘Patricia umemuua mke wangu, kwanini lakini hutaki nifurahi na maisha yangu,nimekosa kuwa na wewe hapo mwanzo,yote uliyonifanyia na Alex umeona haitoshi,umeiondoa Furaha yangu’ ‘Tulia mzee, omba Mungu akuongoze’ ‘Aniongoze wapi tena, kila gumu langu haya sasa nimeachiwa mtoto mchanga, we unaonaje bora nife tu’ ‘Ukifa nani atamlea mtoto wako?’ ‘Sijui, naumia jamani niacheni’Walijitahidi sana kusii lakini wapi Frank aliendelee kulia,wakati anaendelea kulia kumbe Patricia nae alikuwa anakata roho kutokana na mshituko alioupata mara tu alipoingia Frank na kuongea kuhusu kifo cha mke wake. ‘Patricia, Patricia’nesi aliita kwa muda lakini haikusaidia tayari alishakata roho na walipoamua kumpima waliona mapigo ya moyo yamesimama muda mrefu. ********* Umekwenda mke wangu na kuniachia mtoto mdogo,nakupenda sana na naomba huko uliko uniombee nipate nguvu ili niwezi kumlea vizuri mtoto wetu,ntampenda na kumpa anachostahili,naamini wewe ulikuja kunifuta machozi na kweli machozi yangu umeyafuta lakini Mungu baba nae ana makusudi yake,amekuchukua na kuniachia zawadi ya mtoto,ulimwita Glory mi naomba nimwite Clara. Frank aliongea hayo na baada ya kumaliza alitupia udongo kwenye kaburi na kupunga mkono kuashiria kumuaga mke wake na baada ya hapo zege lilianza kushushwa ndani ya kaburi. ****************MWISHO******************* MWISHO WA RIWAYA HII MWANZO WA NYINGINE,KITU "MSAKO" KIKO KWENYE MAANDALIZI YA MWISHO,JUMATATU ITAANZA.
Posted on: Thu, 05 Sep 2013 06:28:31 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015