Samahani kwa wale nitakao wakosea/kuwachefua kulingana na - TopicsExpress



          

Samahani kwa wale nitakao wakosea/kuwachefua kulingana na nilichoakiandika. Si vyema kwa vijana na watu wazima tuliomo mitandaoni kuitumia kutukana matusi ya aina mbalimbali. Mitandao itusaidie kufikisha fikra chanya kwa jamii inayohusika, hili litawavutia wazazi wetu, viongozi wa serikali na wale wa dini kuitemeblea mara kwa mara ili kupata mawazo mbadala kutoka kwa vijana (Taifa la leo). Kama unachangia epuka kuanza na kijembe hii itasaidia kupunguza uchochezi na kuepuka kupotosha maana ya kile kilichoandikwa/ulichoandika. Kama ukianza na kijembe inaweza kutufanya kujali kijembe na kuacha mawazo yako. Humu kuna watu wa aina mbali mbali yaani wasomi, wasio wasomi, vijana, wazee, na viongozi. Hatuwezi kuwa na mawazo yanayofanana kwa kisiasa, kiuchumi na kijamii ikizingatiwa elimu hizo tumezipata sehemu mbalimbali (yaani wengine Ulaya, Asia, America hivyo tuna imani tofauti katika kuendesha mabo kisiasa, kiuchumi na kijamii, hivyo tujifunze kuwa wavumilivu ili tuepuke chuki na uchochezi husio na tija. Mwisho hebu tuwe wabunifu kwa kuandika mambo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yanayojenga na si kubomoa. Mfano kila mtu anaweza kutumia elimu yake au uzoefu katika kuishauri serikali, chama, au taasisi yoyote katika mambo mbalimbali. Hivi vyama vya siasa na dini vimeikuta Tanzania na vitaicha hivyo tusikubali kugawanyika kwa misingi ya dini na siasa. Tanzania ni yetu sote hivyo tushirikiane katika kuijenga na si kubomoa.
Posted on: Wed, 19 Jun 2013 12:51:23 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015