#Swali: Tathmini ya utahini Darasa la #7 #Arusha inaonyesha - TopicsExpress



          

#Swali: Tathmini ya utahini Darasa la #7 #Arusha inaonyesha watahiniwa zaidi ya 1000 hawakufanya mitihani hiyo ya kitaifa mkoani humo shauri ya ujauzito na utoro. Huku tukingoja tathmini toka mikoa mingine ili tupate taswira kamili ya mustakabali wa elimu Tanzania, yabidi tujiulize maswali kadhaa: Moja, nini kifanyike kunusuru vijana hawa? Mbili, kwani #ujauzito na uwezo wa kufanya mitihani vina uhusiano gani? Je, tunapomwambia #mtoto wa #kike asifanye mitihani ati kisa kabeba mimba, hatumnyimi #haki yake ya msingi ya elimu? Nini mtazamo wako katika hili suala?
Posted on: Tue, 12 Nov 2013 07:44:19 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015