2007 tukamaliza chuo, wakati huo Benki hasa Barclays walikuwa na - TopicsExpress



          

2007 tukamaliza chuo, wakati huo Benki hasa Barclays walikuwa na kampeni kubwa ya kupata wateja kwa kuwavutia na mikopo, walijenga mpaka vijiBranchi vya makontena mitaani, walisambaza huduma za kibenki kwa fujo, MPesa na Tigopesa zilikuwa bado. Basi nliograduate nao wakawa na bahati maana wamegraduate wakati benki zinatanusha wigo na kufungua matawi, fasta wakaitwa kuanza kazi, yes, mbuzi kafia kwa muuza supu! Waliopata mabenki, nadhani benki zilijisahau na kushupalia kutafuta wakopaji, kukawa na mianya mingi sana, vijana wakaiona mianya, wakaanza kazi, wakapiga, kuna waliopiga mpaka milioni 800/=. Ghafla kuna kijana alinunua gari 3 zote kwa cash kwa siku 1...Walingara! Leo, 2013, tupo nao hao wapigaji, wana hali tete kama yangu tu, ukiambiwa huyu aliwahi kuwa na 100m/= siku 1 ktk maisha yake, huamini. Tatizo nini? Wazungu wanasema Easy Come, Easy Go. Skia bro, kama ni ngumu kwako kupata 100m/= bila kuiba basi ni NGUMU SANA KWAKO UKIPEWA 100/= KUIZUIA isirudi kuwa Sifuri. Ugumu wa kupata pesa hauufikii ugumu wa kuitunza ama kuiendeleza pesa isikuponyoke. Nani hapa leo hana ratiba ya mtoko, ila akiokota 1m/= hatajikuta Bar jioni? Yes, kikujiacho kiurahisi, basi kitakuponyoka kiurahisi sana. Umekaa hapo job unawaza nini upige siku isogee, basi maisha yako yataishia na fikra hizo hizo, utakuwa mtu wa kuuungaunga mpaka siku utakayoamua kukatunza kasalari kako na kukakuza kazae kijimtaji! Ahsante Fid Q na ile vesi yako kali Usiniite, half-man, niite man and a half, if u think small, and youll remain small for life. . #ImManAndAhalf
Posted on: Wed, 06 Nov 2013 07:19:25 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015