4 wanyongwa nchini Nigeria Wafungwa wanne wamenyongwa kusini mwa - TopicsExpress



          

4 wanyongwa nchini Nigeria Wafungwa wanne wamenyongwa kusini mwa Nigeria, katika kile maafisa wanasema kuwa hukumu ya kwanza ya kunyongwa kutekelezwa kwa miaka saba. Kamishna wa haki katika jimbo la Edo, Henry Idahagbon, aliambia waandishi wa habari kuwa wafungwa hao walinyongwa baada ya kuhukumiwa kifo kwa makosa ya wizi wa mabavu na mauaji. Shirika la Amnesty International lilisema kuwa hatua hiyo ya kuwanyonga wafungwa ni jambo la kuhuzunisha sana kwa watetezi wa haki za binadamu nchini Nigeria. Zaidi ya wafungwa 1,000 nchini Nigeria wanaaminika kuhukumiwa kifo . Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa Rais Goodluck Jonathan hivi karibuni aliwataka magavana wa majimbo kutia saini vibali vya hukumu ya kifo katika jitihada za serikali kupunguza visa vya uhalifu. Bwana Idahagbon alisema kuwa wananume wanne walinyongwa katika gereza la Benin baada ya mahakama kuamuru wanyongwe siku ya Jumatatu.
Posted on: Tue, 25 Jun 2013 16:12:37 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015