ASUBUHI TULIVU LULU ZA INJILI: Mathayo 12:14-21 Hapo Mafarisayo - TopicsExpress



          

ASUBUHI TULIVU LULU ZA INJILI: Mathayo 12:14-21 Hapo Mafarisayo wakatoka, wakashauriana juu yake namna ya kumwangamiza. Yesu alijua hayo, akaondoka huko. Watu wengi wakamfuata naye akawaponya wote lakini akawakataza wasimtambulishe, ili uaguzi wa nabii Isaya utimie, yaani “Mtazameni mtumishi wangu niliyemteua, mpendwa wangu apendezaye moyo wangu. Nitaweka roho yangu juu yake, ili ayatangazie mataifa uadilifu. Hatagombana wala hatapiga kelele, wala hatasikiliza sauti yake barabarani. Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi uwakao bado hatauzima hata aujalie uadilifu kushinda. Mataifa yatategemea jina lake. Je, Somo hili lakufunza nini? MAPOCHOPOCHO: Hii leo twatayarisha Yai la karoti na vitunguu Saumu. Kunayo jinsi unavyotayarisha mlo huu? Nani anayesherekea siku ya kuzaliwa leo? huenda akazawadiwa na KEKI afurahie na wapenziwe. Ungana nami Binti Flo tuamshe kinywa pamoja, ninapokuchezea wimbo uupendao, kukubariki!
Posted on: Sat, 20 Jul 2013 03:10:11 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015