Alichokisema Mtitu kuhusu Filamu za Kanumba hapa nchini# Huu ndio - TopicsExpress



          

Alichokisema Mtitu kuhusu Filamu za Kanumba hapa nchini# Huu ndio ujumbe wa Mtitu#Kwa aibu tulimjibu mheshimiwa rais kuwa marehemu Kanumba hajaacha hata filamu moja, zote ni za msambazaji wake na hata mbili ambazo zilikuwa hazijatoka yaani ‘Ndoa yangu’ na ‘Love & Power’ tayari zilikuwa ni za msambazaji kutokana na aina ya mkataba tunayoingia na msambazaji. Mheshimiwa Rais alisikitika sana, akatuambia kuwa yeye hawezi kutumia nguvu kutukataza kuuza mali zetu lakini angependa kuona kuwa tunamiliki wenyewe filamu zetu na tutakapoona tumekwama tumwambie. Aliongeza kuwa kuuza haki zetu ni kama kuuza utu wetu. Maneno ya mheshimiwa Rais yalinichoma sana. Mimi ni msanii wa kwanza kufanya kazi na kampuni hiyo kama mtayarishaji wa filamu na filamu yao ya kwanza kuisambaza ilikuwa ni ‘Jeraha la Ndoa’ ambayo niliitengeneza mimi. Na kwa kuthibitisha hilo, mwaka huu kampuni hiyo ya Steps ilitoa tuzo ya heshima kwa kampuni yangu ya 5 Effects Movies Ltd kwa ajili hiyo. Nasikitika kukiri kuwa filamu zote ambazo nilizitengeneza kisha zikasambazwa na kampuni ya Steps, siyo zangu tena. Kampuni hiyo imekuwa ikinunua haki zote za filamu wanazopelekewa kwa ajili ya kuzisambaza kwa hiyo baada tu ya kusaini mkataba wao unakuwa huwezi kufaidika tena na chochote kutokana na mauzo au faida nyingine zinazotokana na filamu yako. Unaweza ukashea hii popote pale na wengine wafahamu...!!!!!!!!!!
Posted on: Thu, 19 Sep 2013 22:54:54 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015