BECKHAM AIFAGILIA UINGEREZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA. NGULI wa zamani - TopicsExpress



          

BECKHAM AIFAGILIA UINGEREZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA. NGULI wa zamani wa soka wa Uingereza, David Beckham ameipigia chapuo timu ya taifa ya nchi hiyo kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwakani wakati ikijiandaa kwa ajili ya mechi zake mbili muhimu za mwisho. Uingereza inatarajiwa kupambana na Montenegro na Poland katika Uwanja wa Wembley baadae mwezi huu huku ushindi katika mechi hizo ukiwahakikishia nafasi ya kwenda kushiriki michuano hiyo itakayofanyika nchini Brazil. Kikosi cha Uingereza ambacho kinanolewa na Roy Hodgson kimetoa sare tatu katika mechi tano walizocheza lakini Beckham ambaye ni nahodha wa zamani wa timu hiyo ana uhakika kwamba watasonga mbele. Beckham amesema Uingereza ina wachezaji wengi vijana na pia wako wakongwe kama Frank Lampard na Steven Gerrard hivyo hana shaka na suala la kufuzu.
Posted on: Sat, 05 Oct 2013 17:33:40 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015