Baadhi wa wanafamilia ya Nelson Mandela wanaripotiwa kufungua - TopicsExpress



          

Baadhi wa wanafamilia ya Nelson Mandela wanaripotiwa kufungua mashitaka ya uhalifu dhidi ya mjukuu wake wa kiume, aitwaye Mandla. Msemaji wa polisi ya Afrika ya Kusini wamesema watachunguza tuhuma za kuchezea kaburi kinyume na sheria. Kesi inahusisha miili ya watoto watatu wa rais huyo wa zamani wa Afrika ya Kusini, ambayo inasemekana kuhamishwa kwenye eneo la kuzikiwa la familia hiyo miaka miwili iliyopita. Hapo jana, katika kesi tafauti, mahakama moja iliangalia amri ya kurudishwa kwa mabaki ya miili hiyo kijijini Qunu, ambako watoto hao wa Mandela walizikwa kwenye kiwanja cha familia. Kiongozi huyo wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi kwa sasa yuko kwenye hali mbaya hospitalini mjini Pretoria, anakougua maambukizi kwenye mapafu yake
Posted on: Wed, 03 Jul 2013 08:54:05 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015