Benki ya maendeleo ya Afrika (AFDB) imetoa takwimu mpyA za nchi - TopicsExpress



          

Benki ya maendeleo ya Afrika (AFDB) imetoa takwimu mpyA za nchi zinazoongoza kwa kutembelewa na watalii wachache kwa mwaka. (the least visited African Countries). Ncho hizo ni Chad, DRC, Congo Brazaville, Noger, Afrika ya kati,, Siera Leone, Djibout, Guinea Bissau, Mauritania, Commoro, Sao Tomme&Prince na Guinea ya Ikweta. Nimefarijika kwamba Tanzania haimo katika list lakini nimesikitika kuona nchi zisizo na vivutio kama sisi zikipata watalii wengi kutuzidi. Mauritius inategemea zaidi utalii wa fukwe (beach tourism), na kipitia utalii huo wa fukwe ilipata watalii 965,441 kwa mwaka 2012. Mauritius haina vivutio vya maana zaidi fukwe, ambazo hata Tanzania tunazo. Tena sisi tumewazidi coz wao wana fukwe za bahari tu na sisi tuna fukwe za bahari, maziwa, na mito ambazo tukiziboresha zinaweza kuvutia watalii pia. Lakini wakati Mauritius yenye kutegemea fukwe tu ikipata watalii 965,441 kwa mwaka jana, Tanzania yenye vivutio kedekede ilipata watalii 795,000 tu. Yani tunapata watalii laki 7 tuu wakati tuna Mllima mrefu zaidi Afrika, Mbuga za wanyama, Mito mikubwa, Bahari, Mapori ya akiba, Misitu ya asili, Maziwa makubwa likiwemo ziwa Victoria ambalo ndio ziwa lenye kina kirefu zaidi duniani, Waterfalls, Mabaki ya binadamu wa kale, Historical sites kama Soko la watumwa Zanzibar etc, halafu tunazidiwa na kanchi kanakotegemea utalii wa fukwe tu.! Hii ni Aibu..!! AfBD Fact sheet inaeleza: " Wildlife and Tourism-12 National Parks, the Ngorongoro conservation area, 13 Game reserves, 38 Game Controlled Areas, National Cultural Heritage Sites (about 120 sites), Three large lakes, the Indian Ocean coastline, rivers and wetlands. Potential yield of fish from natural waters is estimated to be 730,000 metric tons annually, present catch is 350,000 metric tons. Forestry and beekeeping non-reserved forest land (1,903.8km2), forest/woodlands with national parks (200km2), and Gazetted forest reserves (1,251.7km2)" Sasa jiulize licha ya vivutio vyote hapo juu bado Tanzania tunazidiwa idadi ya watalii na kanchi kama Mauritius kanakotegemea Beach tu ili kuendesha utalii wake.!! WHAT IS WRONG WITH THIS COUNTRY? NA NINI KIFANYKE??
Posted on: Sun, 15 Sep 2013 08:00:49 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015