Facebook ilibadili katika News Feed, ule muonekano wa picha - TopicsExpress



          

Facebook ilibadili katika News Feed, ule muonekano wa picha unapofungua Facebook ulianza kubadilika. Tangu wakati huo hadi sasa picha zinaonekana kubwa zaidi na pia kwa zile page ulizozipenda nazo zinaonekana kwa upana huku ikikuonyesha kurasa ambazo marafiki zako wamezipenda na kukushauri ubofye “Like”. Hapo ndipo utamu unapokuja. Kuna wale ambao bila kujua walijikuta wame-like kurasa za ngono, na wengi wanadhani marafiki zao hawataona au kugundua kuwa wapo kule. Ubaya wa hii News Feed mpya inatoa mapendekezo kwa marafiki zako nao wazi-like bila kujali ni za kitu gani, ilimradi uwe mtu wa kutembelea mara kwa mara kurasa husika. Kwa wale ambao hawataki kuumbuka mbele ya watu wanaoheshimiana nao nawashauri muwahi mkaangalie ni page gani mmebofya na kama hutaki wajue wewe ni “mwanachama” jitoe au njoo inbox nikuelekeze namfa ya kufanya watu wasizione.
Posted on: Sun, 21 Jul 2013 11:14:32 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015