Falme na ndoto za kiwendawazimu. Inasikitisha sana na ni - TopicsExpress



          

Falme na ndoto za kiwendawazimu. Inasikitisha sana na ni kutojitambua kuona waafrika tungali bado hatujajua ni nani afanywe rafiki na nani afanywe adui,hivi leo tumefikia kutojitambua kiasi kwamba baadhi yetu kudhani tunaweza kuzipeleka nchi za Rwanda na Tanzania katika vita. suala la kujiuliza nani atafaidika na vita hivyo,Ni masikitiko makubwa kwamba siku zote wale ambao hata hawajui kiini cha mgogoro ndio daima huwa waathirika wakubwa wa machafuko. Kimsingi siasa chafu,uchu wa madaraka,ubwana mkubwa wakulinda heshima kwa damu za watu wanyonge,unafiki wa kukumbatia urafiki ghali wa mabwana wakubwa wa kimagharibi ni simu inayoangamiza bara La Africa. Rais Kikwete kwenye hotuba yake iliweka wazi kuwa Tanzania haikuwahi kuwa na sasa sababu za kuingia katika mgogoro na Rwanda,lakini kwa bahati mbaya watu ambao daima huwa na kiu ya kuona umwagaji damu bado hawajaacha chokochoko ya kuunganisha kisa hiki nakile ilimradi kukuza mgogoro. Mfano ni hivi karibuni,tulipopata taarifa kuwa Rwanda ingesitisha utumiaji wa bandari ya Dar es salaam na kwamba wangetumia bandari ya Mombasa ,yalijoteka maoni mbalimbali juu ya swala hilo,lakini cha kutia aibu ni pale wenzetu wengine walipokalia ukweli na kuhisisha tukio hilo na vita vya kiuchumi vya Rwanda dhidi ya Tanzania. Cha kutambua hapa ni kwamba dunia hivi sasa ipo katika ushindani mkubwa wa kibiashara kwa hiyo kama Rwanda inaona itanufaika zaidi kutumia bandari ya Mombasa hakuna haja ya kupiga makelele.....kikubwa ilikuwa ni kuona ni maeneo gani tungeweza kuboresha katika utoaji huduma katika bandari ya Dar es salaam ili kuwa vutivu kwa nchi ya Rwanda na zenginezo,Upo ushahidi na aibu ya kukosa uzalendo kuwa hata baadhi ya wafanya biashara wa Tanzani hupitisha mizigo yao katika bandari ya Mombasa."real its not fair to blame others for your failure!. Ni masikitiko makubwa hata tukio la viongozi wa Kenya,uganda na Rwanda kukaa pamoja na kujadili changamoto zao za kiuchumi,ikiwa ni pamoja na kujenda mtandao wa reli utakaoboresha utoaji huduma na kukuza uchumi wa nchi hizo kuna baadhi yetu tumeibuka na kubeza,badala ya kujifunza na kuona hiyo ni changamoto ya kuikabili katika kutetea nafasi yetu kwenye soko la ushindani la East Africa. mwisho niseme kwamba Adui wetu wa kwanza kuanza kupigana naye vita ni fikra na dhamira zetu...na si vinginevyo. Br KAPONA
Posted on: Wed, 28 Aug 2013 07:30:21 +0000

Recently Viewed Topics




© 2015