Ferguson awaponza marefa Uingereza Anaweza kuwa ameshastaafu, - TopicsExpress



          

Ferguson awaponza marefa Uingereza Anaweza kuwa ameshastaafu, lakini aliyekuwa kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson bado ana uzito na sasa amewaponza waamuzi. Mmoja wao, Mark Halsey amedai kwamba ilikuwa kawaida kwao kuwasiliana na Fergie kwa ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) na sasa wameonywa juu ya tabia hiyo isiyovumilika. Halsey naye alistaafu kama fergie mwishoni mwa msimu uliopita, ambapo kauli yake imeshitua wadau wengi wa soka, ikizingatiwa kwamba Ferguson na Manchester walikuwa wakishutumiwa kwa kupata matokeo ya kushinda katika wakati na namna ya kushangaza. Halsey anadai kwamba alipata kuwasiliana na Fergie binafsi katika suala zima la kuungana mkono. Mwamuzi huyo aliandika pia juu ya utata uliotokea dhidi ya mwamuzi mwenzake, Mark Clattenburg aliyedaiwa kumbagua mchezaji wa Chelsea John Obi Mikel, na akadai kwamba aliwasiliana na Fergie pia ili kupata kuungwa mkono naye. “Nilibeba jukumu hilo mwenyewe nikampigia simu Sir Alex na kumwomba kulizungumzia. Alikubali na kutumia mkutano wake wa Ijumaa na waandishi wa habari kusema hadharani kwamba Mark asingeweza kusema mambo ya kukashifu kama yaliyodaiwa na Mikel na Chelsea. Kwa jinsi mambo yalivyokuwa, kauli yake ilisaidia sana,” akasema mwamuzi huyo. Hata hivyo, alikiri kwamba ilichukua muda mrefu kuweza kumshawishi Fergie kuwa upande wake na kisha walikuwa na uhusiano mzuri sana.
Posted on: Tue, 17 Sep 2013 03:42:14 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015