HABARINI WADAU KAMA KAWAIDA LEO NDO SIKU ILE AMBAYO TUNAANZA NA - TopicsExpress



          

HABARINI WADAU KAMA KAWAIDA LEO NDO SIKU ILE AMBAYO TUNAANZA NA STORY YETU TOLEO LA KWANZA. JINA LA STORY--#UKUBWA_DAWA. MTUNZI---#mfikwa j Asubuhi tulivu jua linapambazuka ndege wa angani wanalilia kwa furaha miti na wengine wanarukaruka juu angani ni katika kijiji kimoja kilichopo mkoa wa Iringa wilaya ya iringa vijijini kinaitwa NDULI. Katika kijiji hicho kulikuwa na familia mbili ambazo ni ya kwanza ni familia ya mzee Mfikwa na ya pili ni famailia ya mzee Thomas katika familia hizi familia ya mzee Mfikwa alikuwa na mke ambae anaitwa Elizabeth na watoto wawili ambao ni JJ mwenye miaka 21 na Janeth mwenye miaka 15 na pia katika familia ya mzee Thomas yeye alikuwa na mke aitwae Rose na mtoto mmoja aitwae K2 kijana mwenye miaka 23.Ni familia ambazo zilikuwa na maisha duni sana lakini katika familia hizo hawakuweza kutengana na walikuwa na ushirikiano sana kwa kila shida na raha.Ilikuwa jumatatu ya tarehe 01.10.2001 majira ya saa mbili asubuhi JJ mtoto wa mzee Mfikwa alikuwa anaenda polini kuwinda maana yeye alikuwa anapenda sana kuwinda wanyama pori wakati akiwa anaenda porini alipita nyumbani kwa mzee TAhomas kwa ajili ya kuwajulia hali alipofika kwa mzee Thomas alibisha hodi na kuingia ndani akawasalimia wote lakini kabla ajaaga kuondoka ndipo alipomuuliza K2 fariki yangu vipi mwenzio naenda zangu porini kuwinda angalau leo nikapate kitoweo K2 alicheka sana kwa maana yeye alikuwa ni mtu mvivu sana yani yeye ni kula kulala baada ya kumwambia hivyo JJ akamwambia K2 rafiki yangu mbona unacheka kwanini K2 akamwambia nakucheka kwa sababu kila siku unaenda porini lakini cha kushangaza wanyama unaokamata ni sungura tu kwanini siku nyingine usiwe unawinda swala,digidigi nk na wanyama wakubwa JJ akamwambia rafiki yangu unanifurahisha sana unajua kuwinda ni swala dogo sana si ndio twende ukajaribu uone jinsi ilivyo kuwa ngumu kuwinda siyo kazi ndogo rafiki yangu K2 akamwambia mwenzie acha ubababishaji leo twende tukawinde uone sasa mambo yangu ya polini wakatoka safari ikaanza kabla hawajafika kama kilomita mbili hivi K2 akamwambia rafiki yake JJ ninawazo maana kila siku mwenzio narifikiria sipati jibu ebu mwenzangu nishauri huku wakiwa wanatembea K2 ndipo alipoanza kumwambia JJ kuwa rafiki yangu unajua fika kama familia zetu zinamisha duni sana na ukiangalia sisi ndo vijana wakubwa katika familia hizi ubaya zaidi mwenzangu una mdogo wako anaitwa Janeth kwanza ndo anamaliza elimu ya shule ya msingi na wewe ndo unaonekana ndo tegemeo katika familia yako na dada yako anakutegemea wewe ndo umsomeshe elimu ya sekondari pindi atakapo maliza shule kwa sababu baba yako kwa sasa hana tena fedha za kuwendeleza shule na mimi kwetu hali kama unavyo iona je mwenzangu unafikiria nini? JJ aliguna kisha akamwambia rafiki yangu uliyosema ni kweli lakini hata sijui nifanye nini ila kwa kuwa wewe ndo umeanza kusema mada hii ebu nipe wazo mwenzangu ambalo litafungua ubongo wangu K2 akamwambia sasa sikia hapa cha kufanya inabidi kwende mkoa mwingine tukajaribu bahati zetu maana hapa kijijini si unajua hapana kitu JJ alishtuka kisha akasema sasa tukitoka hapa kijijini na wazazi wetu watakuwa wanawasaidia wakina nani k2 alicheka sana kisha akamwambia rafiki yake ebu kuwa mkubwa rafiki yangu wewe umelelewa na nani si wazazi wako kwani sasa acha utoto wewe twende tukatafute maisha sehemu nyingine waliendelea na safari yao. Baada ya siku kadhaa kupita K2 alienda kwa rafiki yake JJ kufika njiani alikutatana na JJ nae alikuwa anaenda kwake ndipo walipokutana njiani alitafuta sehemu ili wapange wataondoka vipi pale kijijini kwao K2 akamwambia rafiki yake mwenzio napenda twende Dar es saalam pale najua maisha yako poa sana na JJ akamwambia mimi napenda Kigoma si unajua kigoma kuna ziwa tanganyika tena kule tunaweza kuvua samaki kama tukikosa kazi kabisa au mwenzangu unasemaje kwa kuwa K2 nia yake ni kutoka pale kijijini walikubaliana kuwa wakatafute maisha mkoa wa kigoma alipanga safari yao walipomaliza ikabidi kila mmoja arudi kwao kuwaambia wazazi wote walifanya hivyo. Safari ilianza kuelekea mkoa wa kigoma kwa kuwa pale kijijini kwao kuna njia ya mkato walipanda basi toka nduli na kuelekea mkoa wa Dodoma alipofika mkoa wa Dodoma walikaa pale kama siku mbili baada ya siku mbili walipata usafiri wa treni hadi mkoani Kigoma kwa kuwa safari walianza mchana kigoma alifika kama saa nne usiku ikabidi walale mulemule kwenye treni mpaka kesho yake. Kulipambazuka siku inayofuata na wakaanza kushangaa mjini na walikuwa hawajui waende wapi K2 kwa kuwa alikuwa mjanja akamwambia rafiki yake sikia hapa twende kwanza stendi ya mabasi maana pale lazima tutakutana na vijana wengi na tutajua tuanzie wapi.Kigoma ni mji ambao ulikuwa umechafuka sana wizi ulilindima ujambazi ndo usiseme watu wanauawa ovyo kila kona ni uharifu Polisi mkoa wa kigoma ulikuwa umeanzisha operation maalum siku hiyo kamata kamata maeneo mbalimbali. Mchana wa tarehe 02.11.2001 K2 na JJ alifika stend ya mabasi na kutembea tembea hawajui waanzie wapi wamalizie wapi kwa kuwa walikuwa wamevaa rafu sana kila mtu alijua ni machokorahaa mara baada ya muda mfupi Polisi walifika maeneo ya stendi wapiga debe wanaozurula pasipo msingi wowote walikamatwa watu mbio zilishamiri JJ na rafiki yake K2 nao waliona hapa siyo kwa kukaa walianza mbio bahati mbaya wakati wanakimbia na JJ kwa kuwa alikuwa hana mbio ndipo alipofanikiwa kukamatwa na askali polisi na K2kwa kuwa alikuwa ana mbio aliweza kukimbia na kumuacha rafiki yake amekatwa na polisi. Polisi walipomaliza kukamata eneo lile watuhumiwa wote walipelekwa kwanza kituo cha polisi kwa maojiano zaidi ili wapelekwe mahakamani. JE JJ ALIPELEKWA MAHAKANI NA JE K2 ALIKIMBILIA WAPI? Usikose toleo la pili la stori hii
Posted on: Thu, 03 Oct 2013 05:07:38 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015