HIVI ZANZIBAR HAIWEZI KUTOA MAKATIBU WAKUU? Mabadiliko - TopicsExpress



          

HIVI ZANZIBAR HAIWEZI KUTOA MAKATIBU WAKUU? Mabadiliko yaliyofanywa kwa upande wa makatibu wa wakuu ni kama ifuatavyo; Dk. Florens Turuka amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Joyce Mapunjo Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jumanne Sagini amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Dk. Servacius Likwalile amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Patrick Makungu amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Alphayo Kitanda amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Shaaban Mwinjaka amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dk.Uledi Mussa amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Profesa Sifuni Mchome amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Charles Pallangyo amekuwa Katibu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Anna Maembe amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sihaba Nkinga amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sophia Kaduma amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika. Peniel Lyimo ambaye anahamia Ofisi ya Rais - Ikulu kwenye ‘Presidential‘s Delivery Bureau’ kama Naibu Mtendaji Mkuu mwenye jukumu la kuanzisha na kuongoza Idara ya Mageuzi ya Kilimo mwanzoni alikuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu. Aidha Balozi Sefue alisema Rais Kikwete pia amefanya uteuzi wa naibu makatibu wakuu wapya na kuwapa uhamisho baadhi yao. Angelina Madete Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Regina Kikuli Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Zuberi Sumataba Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI - anayeshughulikia suala la elimu katika ngazi za Serikali za Mitaa, Edwin Kiliba Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI, Deodatus Mtasiwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI ambaye atashughulikia saula la afya upande wa Serikali za Mitaa, Dk. Yamungu Kayandabila amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Adolf Mkenda Naibu Katibu Mkuu ya Fedha anayeshughulikia Sera, Dorothy Mwanyika Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha anayeshughulikia Fedha za Nje na Madeni, Rose Shelukindo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Selassie Mayunga Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Monica Mwamunyange Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Consolata Mgimba Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Profesa Elisante ole Gabriel Laizer amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Armantius Msole Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, John Mngondo ambaye amehamishiwa Wizara ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Selestine Gesimba amehamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii anatoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Injinia Ngosi Mwihava anahamia Wizara ya Nishati na Madini kutokea Ofisi ya Makamu wa Rais, Maria Bilia amehamia Wizara ya Viwanda na Biashara kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Nuru Milao anahamia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.
Posted on: Thu, 22 Aug 2013 05:45:18 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015