Hali zenu, wajukuu zangu?... Napenda kutumia fursa hii kwa - TopicsExpress



          

Hali zenu, wajukuu zangu?... Napenda kutumia fursa hii kwa kuwafahamisha yakuwa nimehamia huku kwa Mama Chonya… Kwa wale watakaotaka kuja kuniona, sio mbaya nikiwaelekeza: uje wewe na rafiki yako si mbaya hata mkija 20 hapa nyumbani kwangu… Ili ufike hapa nyumbani kwangu, panda gari la Gongo La Mboto, shuka Gongo La Mboto mwisho… Halafu chukua magari ya Pugu-Kajiungeni, shuka mwisho wa gari, halafu panda vigari vya kwenda Kisarawe, teremka kwa Njovu… Ukifika kwa Njovu, chukua Bajaj, mwambie dereva wa Bajaj akulete kwa mama Zai… Ukifika kwa Mama Zai, panda pikipiki mpaka Kisarawe Social Hall…Ukifika hapo kuna baiskeli, mwambie akulete hadi Uwanja wa Fakhi… Ukifika hapo Uwanja wa Fakhi, angalia mbele kuna sheli, pita kichochoro mbele utaiona shule ya msingi Ndama…. Nyuma ya shule utaona gari bovu, kunja kulia, utashuka na hiyo kona hadi karibu na kilima utaona duka kushoto halafu kuna kokoto… Ukifika hapo, ulizia jamaa wa hapo kilingeni wakulete kwa Mama Chonya... Hao jamaa watakuacha njia panda kuna kimfereji… Vuka huo mfereji na nyumba ya 8 ndio nyumba yangu, mpya kabisa, nimehamia jana ! Karibuni nyumbani kwangu, wajukuu zangu !... #Via #AdminKibongobongo
Posted on: Tue, 24 Sep 2013 20:57:15 +0000

Trending Topics



>
Game Recognizes Game As Carmelo Makes His First VC Plays
6/22/2014 Soulful Sunday another chance to hear the origins of

Recently Viewed Topics




© 2015