Hamas kuendeleza muqawama dhidi ya Israel Na Mahmoud Zahar mmoja - TopicsExpress



          

Hamas kuendeleza muqawama dhidi ya Israel Na Mahmoud Zahar mmoja wa viongozi waandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas amesisitiza juu ya kufungamana harakati hiyo na muqawama dhidi ya utawala wa wa Israel. Akihutubia maelfu ya wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya serikali iliyochaguliwa na wananchi ya Palestina huko Khan Yunes katika eneo la kusini mwa Ukanda wa Gaza , Mahmoud az Zahar mjumbe wa ofisi ya kisiasa na mbunge wa Bunge la Palestina amesisitiza kuwa, Hamas bado haijaacha mapambano yake ya muqawama dhidi ya Israeil na wala haitatoa mwanya kwa mtu yeyote kuisambaratisha azma hiyo ya wananchi wa Palestina. Kiongozi huyo wa Hamas amesema kuwa, Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina hana ubavu na nguvu za kusimamisha mazungumzo ya amani na Israel. Ameongeza kuwa, suala la kukombolewa ardhi za Palestina halina mjadala na Hamas katika kipindi cha miaka 6 iliyopita iliingia mara 4 kwenye vita dhidi ya majeshi ya Israel na wala haikushindwa kwenye vita hivyo.
Posted on: Sat, 05 Oct 2013 07:11:20 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015