IMPORTANT FOR ALL US - RWANDA - TopicsExpress



          

IMPORTANT FOR ALL US - RWANDA BREAKINGNEWS #KAMPALA_PEACETALKS_YANGOA_NANGA_TANGU_SEPTEMBER_TANU_2013 KATI YA SERIKALI YA KINSHASA NA KUNDI LA WAPIGANAJI WA M23!||Habari zipatikanazo kwa mtandao wa ICIGRL zinasema kwamba Rais wa Uganda,pia Mkuu wa Conferance ya nchi za maziwa makuu,Luteni Jeneral Yoweli Kaguta Museveni amealika mkutano maarumu wa ma Rais wenzake miongoni mwao ni Rais: Paul Kagame wa Rwanda,Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania,Rais Kenyatta Uhuru wa Kenya,Major General Peter Nkurunziza wa Burundi,General Sassou Ngueso wa Congo Brazzaville,Salva Kiir wa Sudani ya Kusini,José Edouardo de Santos wa Angola,Dr Banda wa Malawi,Michael Sata wa Zambia pia General Joseph Kabila atahuzulia mkutano huo wenye lengo la kufufuwa mazungumzo ya Kampala .Kitambo wiki jana,kuna fununu zinazosema kwamba kwa ajiri ya Mkutano huu ,Rais Museveni aliwasihi Chama cha M23 warudi nyuma toka maeneo walioyashikiria kando na muji wa Goma na viunga vyake ili watimizi kilometa 20 nje na muji huu kama ilivo mkataba wa Kampala Talehe 24 November mwaka jana.Wanadisi wa mambo wanasema kwamba huenda ni Katika mkutano huo ma Rais wa Rwanda na Tanzania watajalibu kuumaliza mgogoro kati ya nchi hizo jirani Kufuatilia matamshi ya Jakaya Kikwete kwa kuomba Rwanda kuzungumza na wanamugambo wa FD5R waliofanya mauwaji ya kikatili nchini Rwanda kabla ya kupewa hifadhi na nchi jirani ya Kongo miaka 20 inapita,pendekezo Rwanda ilitupilia mbali kwa maneno makali kwamba yeyote atakaejalibu kuwaunga mkono wa FDLR ataandamwa vikali na kumuangamiza sana .Upande wa M23 nao wasemekana kuongeza nguvu ndani ya Ujumbe wake huko Kampala Speke Hotel wakiwajumlisha Buana Amani Kabasha,huu ni Msemaji wa kundi la M23 ,Tawi la siasa na pia Mhandisi Ben Mbonimpa ,Katibu mtendaji wa chama cha M23,kwa kuwaunga mkono team ya Rene Abandi,ambao wanaakaa huko tangu miezi mnne .Je,kuna matumaini kwa mavuno bora kuhusu mkutano huu? Hebu tuma maoni yako ao komenti bila wasi wasi.Vijana wa Kigali,Kinshasa,Kampala,Dar es salam ,Nairobi,Buja,Brazza ,Djuba,Bryntyre,Luanda ,Nairobi #MNALISEMEAJE?[Imeandikwa na RBN kutoka Kigali,kwa kushirikiana na Marshall Greatlakes Newline toka jijini Mbarara,Uganda,leo September 1 2013,at 16:25 Majila ya GMT]
Posted on: Sun, 01 Sep 2013 18:28:35 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015