JUMAPILI YA 22 YA MWAKA C WA - TopicsExpress



          

JUMAPILI YA 22 YA MWAKA C WA KANISA Masomo 1.Ybs.3:17-20,28-29 2.Ebr.12:18-19,22-24 3.Lk.14:1,7-14 Wapendwa wana wa Mungu,nawakaribisheni katika umoja wenu kama sehemu ya Taifa la Mungu katika Dominika hii ya 22 ya mwaka C wa Kanisa,ili tutafakari Neno la Mungu.Msingi wa Tafakari yetu ni Somo la Kwanza na kwa namna ya pekee,maneno yatokayo katika Kitabu cha Ybs 3:18, “Kadiri ulivyo mkubwa ndivyo ujinyenyekeshe;nawe utapata neema mbele za Bwana”,Na pia maneno yatokayo katika Injili ya Luka 14:11, “Kwa maana kila ajikwezaye atashushwa na kila ajishushaye atakwezwa”. Bwana wetu Yesu Kristo,aliye kielelezo chetu cha safari yetu ya kufika mbinguni alikuwa wa kwanza kuuishi Unyenyekevu,rejea Wafilipi 2:6,Kristo ambaye ijapokuwa alikuwa namna ya Mungu,hakuchukulia kwamba kuwa sawa na Mungu lilikuwa jambo la kushikamana nalo.” Kwa tendo hilo la Kristo,anatufundisha kwamba unyenyekevu sio unyonge na wala sio ujinga bali ni kwa njia ya unyenyekevu tunaweza kuwafikia wenzetu zaidi na kuwa watu wa msaada zaidi kwao. Bila shaka tutakubaliana kwamba kinyume cha unyenyekevu ni kiburi na majivuno.Hata hivyo,tutajuaje kama tuna kiburi? • Mwenye kiburi huona tu mema aliyo nayo na atendayo na hufumbia macho kasoro,vilema na mapungufu yake mwenyewe • Mwenye kiburi hataki kusahihishwa au kukosolewa • Mwenye kiburi anapenda kujisifu na kujigamba • Mwenye kiburi hayupo tayari kutambua kwamba nguvu,akili na uwezo alio nao umetokana na Mungu Hata hivyo hatuna budi tujue katika maisha ya kawaida,chanzo cha kiburi kwa tulio wengi ni nini? • Mafanikio katika nyanya mbalimbali za kimaisha(kiuchumi,kiafya,kisiasa,kijamii)n.k Ikumbukwe kwamba kikwazo kikubwa katika kuingia katika ufalme wa Mungu,ni ile hali ya kujiona tunafaa mbele ya Mungu na hatuhitaji marekebisho yoyote katika nafsi zetu.Turejee maneno ya Kristo;Mathayo 21:31; “Watoza Ushuru na malaya watakuwa wa kwanza katika kuingia Ufalme wa Mungu”.Na mtume Paulo,anasema hamna anayeweza kudai kwamba Ufalme wa Mungu anaweza kuupata kutokana na mastahili yake,rejea Warumi 3:21-31 na Wagalatia 2:16-21 Kutokuwa na unyenyekevu kunaleta ugumu kama sio kuwezekana kabisa kuiishi Amri ya Mapendo.Kristo kutokana na unyenyekevu wake aliwapenda watu wote bila kujali jinsia,mali,uwezo wa kiakili wa watu na kadhalika.Kristo akitambua nafasi ya Unyenyekevu katika kuyaishi mapenzi ya Mungu,leo anatoa angalisho kwamba,kuna hatari ya wale wenye chochote,kuwaalika matajiri tu kwenye sherehe zao;ni ngumu kwa mtu ambaye sio Mnyenyekevu kuingia kwenye nyumba ya ambaye sio tajiri na kumwalika,rejeeni maisha ya kawaida tunayoishi,mintaarafu mialiko ya sherehe za wale tunaowaita wakubwa kwa kadiri ya hekima ya kibinadamu. Swali kubwa la kujiuliza,tumefanya nini pale tulipopata mafanikio katika maisha yetu?Kila mtu kadiri ya nafasi yake,ajiulize;mfanya biashara,kiongozi,na kadhalika.Tufanye tathmini iwapo kama nafasi zetu zinatufanya tuwatenge wenzetu,tuwanyanyase na kuwaona wengine kama sio binadamu kamili.Hatuna budi kujua kwamba yote tuliyona nayo yametoka kwa Mungu na hivyo sifa na utukufu ni wake na sio wetu. Unyenyekevu wa kweli sio kitu au jambo litokalo nje ya nafsi ya mtu bali ndani ya nafsi ya mtu.Mtu mnyenyekevu anajiona yeye ni nani mbele ya Mungu?Vipaji vyake na maweza yake anajua kabisa kwamba mpaji ni Mungu!Sambamba na hilo ni kwa fadhila ya unyenyekevu,tunajua maweza na mapungufu yetu na kumuomba msamaha Mungu kwa dhambi zetu.Mtu mnyenyekevu ni rahisi kuona wapi amemkosea Mungu na jirani yake! Tuombe neema ya Mungu ili tuweze kuwa na fadhila ya unyenyekevu! Prepared by Rev.Father Furaha Aggrey Ntasamaye JUMAPILI YA 22 YA MWAKA C WA KANISA Masomo 1.Ybs.3:17-20,28-29 2.Ebr.12:18-19,22-24 3.Lk.14:1,7-14 Wapendwa wana wa Mungu,nawakaribisheni katika umoja wenu kama sehemu ya Taifa la Mungu katika Dominika hii ya 22 ya mwaka C wa Kanisa,ili tutafakari Neno la Mungu.Msingi wa Tafakari yetu ni Somo la Kwanza na kwa namna ya pekee,maneno yatokayo katika Kitabu cha Ybs 3:18, “Kadiri ulivyo mkubwa ndivyo ujinyenyekeshe;nawe utapata neema mbele za Bwana”,Na pia maneno yatokayo katika Injili ya Luka 14:11, “Kwa maana kila ajikwezaye atashushwa na kila ajishushaye atakwezwa”. Bwana wetu Yesu Kristo,aliye kielelezo chetu cha safari yetu ya kufika mbinguni alikuwa wa kwanza kuuishi Unyenyekevu,rejea Wafilipi 2:6,Kristo ambaye ijapokuwa alikuwa namna ya Mungu,hakuchukulia kwamba kuwa sawa na Mungu lilikuwa jambo la kushikamana nalo.” Kwa tendo hilo la Kristo,anatufundisha kwamba unyenyekevu sio unyonge na wala sio ujinga bali ni kwa njia ya unyenyekevu tunaweza kuwafikia wenzetu zaidi na kuwa watu wa msaada zaidi kwao. Bila shaka tutakubaliana kwamba kinyume cha unyenyekevu ni kiburi na majivuno.Hata hivyo,tutajuaje kama tuna kiburi? • Mwenye kiburi huona tu mema aliyo nayo na atendayo na hufumbia macho kasoro,vilema na mapungufu yake mwenyewe • Mwenye kiburi hataki kusahihishwa au kukosolewa • Mwenye kiburi anapenda kujisifu na kujigamba • Mwenye kiburi hayupo tayari kutambua kwamba nguvu,akili na uwezo alio nao umetokana na Mungu Hata hivyo hatuna budi tujue katika maisha ya kawaida,chanzo cha kiburi kwa tulio wengi ni nini? • Mafanikio katika nyanya mbalimbali za kimaisha(kiuchumi,kiafya,kisiasa,kijamii)n.k Ikumbukwe kwamba kikwazo kikubwa katika kuingia katika ufalme wa Mungu,ni ile hali ya kujiona tunafaa mbele ya Mungu na hatuhitaji marekebisho yoyote katika nafsi zetu.Turejee maneno ya Kristo;Mathayo 21:31; “Watoza Ushuru na malaya watakuwa wa kwanza katika kuingia Ufalme wa Mungu”.Na mtume Paulo,anasema hamna anayeweza kudai kwamba Ufalme wa Mungu anaweza kuupata kutokana na mastahili yake,rejea Warumi 3:21-31 na Wagalatia 2:16-21 Kutokuwa na unyenyekevu kunaleta ugumu kama sio kuwezekana kabisa kuiishi Amri ya Mapendo.Kristo kutokana na unyenyekevu wake aliwapenda watu wote bila kujali jinsia,mali,uwezo wa kiakili wa watu na kadhalika.Kristo akitambua nafasi ya Unyenyekevu katika kuyaishi mapenzi ya Mungu,leo anatoa angalisho kwamba,kuna hatari ya wale wenye chochote,kuwaalika matajiri tu kwenye sherehe zao;ni ngumu kwa mtu ambaye sio Mnyenyekevu kuingia kwenye nyumba ya ambaye sio tajiri na kumwalika,rejeeni maisha ya kawaida tunayoishi,mintaarafu mialiko ya sherehe za wale tunaowaita wakubwa kwa kadiri ya hekima ya kibinadamu. Swali kubwa la kujiuliza,tumefanya nini pale tulipopata mafanikio katika maisha yetu?Kila mtu kadiri ya nafasi yake,ajiulize;mfanya biashara,kiongozi,na kadhalika.Tufanye tathmini iwapo kama nafasi zetu zinatufanya tuwatenge wenzetu,tuwanyanyase na kuwaona wengine kama sio binadamu kamili.Hatuna budi kujua kwamba yote tuliyona nayo yametoka kwa Mungu na hivyo sifa na utukufu ni wake na sio wetu. Unyenyekevu wa kweli sio kitu au jambo litokalo nje ya nafsi ya mtu bali ndani ya nafsi ya mtu.Mtu mnyenyekevu anajiona yeye ni nani mbele ya Mungu?Vipaji vyake na maweza yake anajua kabisa kwamba mpaji ni Mungu!Sambamba na hilo ni kwa fadhila ya unyenyekevu,tunajua maweza na mapungufu yetu na kumuomba msamaha Mungu kwa dhambi zetu.Mtu mnyenyekevu ni rahisi kuona wapi amemkosea Mungu na jirani yake! Tuombe neema ya Mungu ili tuweze kuwa na fadhila ya unyenyekevu! Prepared by Rev.Father Furaha Aggrey Ntasamaye JUMAPILI YA 22 YA MWAKA C WA KANISA Masomo 1.Ybs.3:17-20,28-29 2.Ebr.12:18-19,22-24 3.Lk.14:1,7-14 Wapendwa wana wa Mungu,nawakaribisheni katika umoja wenu kama sehemu ya Taifa la Mungu katika Dominika hii ya 22 ya mwaka C wa Kanisa,ili tutafakari Neno la Mungu.Msingi wa Tafakari yetu ni Somo la Kwanza na kwa namna ya pekee,maneno yatokayo katika Kitabu cha Ybs 3:18, “Kadiri ulivyo mkubwa ndivyo ujinyenyekeshe;nawe utapata neema mbele za Bwana”,Na pia maneno yatokayo katika Injili ya Luka 14:11, “Kwa maana kila ajikwezaye atashushwa na kila ajishushaye atakwezwa”. Bwana wetu Yesu Kristo,aliye kielelezo chetu cha safari yetu ya kufika mbinguni alikuwa wa kwanza kuuishi Unyenyekevu,rejea Wafilipi 2:6,Kristo ambaye ijapokuwa alikuwa namna ya Mungu,hakuchukulia kwamba kuwa sawa na Mungu lilikuwa jambo la kushikamana nalo.” Kwa tendo hilo la Kristo,anatufundisha kwamba unyenyekevu sio unyonge na wala sio ujinga bali ni kwa njia ya unyenyekevu tunaweza kuwafikia wenzetu zaidi na kuwa watu wa msaada zaidi kwao. Bila shaka tutakubaliana kwamba kinyume cha unyenyekevu ni kiburi na majivuno.Hata hivyo,tutajuaje kama tuna kiburi? • Mwenye kiburi huona tu mema aliyo nayo na atendayo na hufumbia macho kasoro,vilema na mapungufu yake mwenyewe • Mwenye kiburi hataki kusahihishwa au kukosolewa • Mwenye kiburi anapenda kujisifu na kujigamba • Mwenye kiburi hayupo tayari kutambua kwamba nguvu,akili na uwezo alio nao umetokana na Mungu Hata hivyo hatuna budi tujue katika maisha ya kawaida,chanzo cha kiburi kwa tulio wengi ni nini? • Mafanikio katika nyanya mbalimbali za kimaisha(kiuchumi,kiafya,kisiasa,kijamii)n.k Ikumbukwe kwamba kikwazo kikubwa katika kuingia katika ufalme wa Mungu,ni ile hali ya kujiona tunafaa mbele ya Mungu na hatuhitaji marekebisho yoyote katika nafsi zetu.Turejee maneno ya Kristo;Mathayo 21:31; “Watoza Ushuru na malaya watakuwa wa kwanza katika kuingia Ufalme wa Mungu”.Na mtume Paulo,anasema hamna anayeweza kudai kwamba Ufalme wa Mungu anaweza kuupata kutokana na mastahili yake,rejea Warumi 3:21-31 na Wagalatia 2:16-21 Kutokuwa na unyenyekevu kunaleta ugumu kama sio kuwezekana kabisa kuiishi Amri ya Mapendo.Kristo kutokana na unyenyekevu wake aliwapenda watu wote bila kujali jinsia,mali,uwezo wa kiakili wa watu na kadhalika.Kristo akitambua nafasi ya Unyenyekevu katika kuyaishi mapenzi ya Mungu,leo anatoa angalisho kwamba,kuna hatari ya wale wenye chochote,kuwaalika matajiri tu kwenye sherehe zao;ni ngumu kwa mtu ambaye sio Mnyenyekevu kuingia kwenye nyumba ya ambaye sio tajiri na kumwalika,rejeeni maisha ya kawaida tunayoishi,mintaarafu mialiko ya sherehe za wale tunaowaita wakubwa kwa kadiri ya hekima ya kibinadamu. Swali kubwa la kujiuliza,tumefanya nini pale tulipopata mafanikio katika maisha yetu?Kila mtu kadiri ya nafasi yake,ajiulize;mfanya biashara,kiongozi,na kadhalika.Tufanye tathmini iwapo kama nafasi zetu zinatufanya tuwatenge wenzetu,tuwanyanyase na kuwaona wengine kama sio binadamu kamili.Hatuna budi kujua kwamba yote tuliyona nayo yametoka kwa Mungu na hivyo sifa na utukufu ni wake na sio wetu. Unyenyekevu wa kweli sio kitu au jambo litokalo nje ya nafsi ya mtu bali ndani ya nafsi ya mtu.Mtu mnyenyekevu anajiona yeye ni nani mbele ya Mungu?Vipaji vyake na maweza yake anajua kabisa kwamba mpaji ni Mungu!Sambamba na hilo ni kwa fadhila ya unyenyekevu,tunajua maweza na mapungufu yetu na kumuomba msamaha Mungu kwa dhambi zetu.Mtu mnyenyekevu ni rahisi kuona wapi amemkosea Mungu na jirani yake! Tuombe neema ya Mungu ili tuweze kuwa na fadhila ya unyenyekevu! Prepared by Rev.Father Furaha Aggrey Ntasamaye
Posted on: Sat, 31 Aug 2013 20:20:59 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015