Jogoo la kwanza linawika bado nipo emani ,gunia nimejifunika na - TopicsExpress



          

Jogoo la kwanza linawika bado nipo emani ,gunia nimejifunika na mbavu zangu mkekani,hewani sauti zinasikika sijui ni viumbe gani siwezi sema shetani kwa kuwa sina uhakika,naamka kisha nakaa bado giza totoro tumboni nahisi njaa nakitamani kiporo nachukua kiberiti ili niwashe kibatari ooh shit hakina njiti na scut natafakari,nusu saa baadae mwangaza unanyemelea naona nijiandae nisikae kutegemea,mbu wananiwinda kunguni panya na chawa naamini nitashinda haina haja ya kuchachawa.
Posted on: Sun, 18 Aug 2013 04:34:24 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015