KAGAME NA MUSEVENI - HATARI SANA KWA TAIFA LETU! Uharamia - TopicsExpress



          

KAGAME NA MUSEVENI - HATARI SANA KWA TAIFA LETU! Uharamia anaoufanya Kagame kule Mashariki ya Congo hapa kwetu alifanikiwa siku nyingi. Tofauti ya DRC Mashariki na mikoa yetu ya Kagera na Kigoma ni kwamba wenzetu wanayo hata majeshi ya mgambo ya uzalendo wao yanayotetea ardhi yao na uhuru wao, kama vile Mai Mai. Lakini sisi tuliuawa kabisa uhanga wetu kwa ajili ya Nchi yetu. Tumebaki kuwasujudia wageni wanaoteka na kuipora nchi yetu, na kututia utumwani katika nchi yetu wenyewe. Hii ndiyo raha ambayo Nyerere aliwaandalia Kagame na Mseveni kwa Watanganyika. Kagame tayari ameingiza katika Nchi yetu Wanyarwandazaidi ya 35,000 wenye silaha, wengi wakiwa katika mapori ya Hifadhi ya Taifa ya Buligi na maelfu ya ng’ombe waliowaingiza kutoka kwao Rwanda na Uganda. Kwani kule kwao wamejiwekea sheria kali ya kuokoa mazingira yao, kwamba ni marufuku mtu kumiliki zaidi ya ng’ombe tano (5). Kwahiyo mamia ya maelfu ya ng’ombe zao wameziingiza katika ardhi yetu kwa njia za porini, na wapo Wanyarwanda wenye ng’ombe mpaka 10,000 mtu mmoja ndani ya Nchi yetu. Maelfu mengi ya ng’ombe hao wa Wanyarwanda wanajulikana kuwa mali ya dikteta Paul Kagame mwenyewe na mawaziri wake, na wengine ni mali ya dikteta Yoweri Mseveni, wengi wakiwa hata na mihuri ya NRA! Mbali ya Hifadhi ya Taifa ya Buligi, maelfu mengi ya ng’ombe wao wamewaswagia katika mapori yetu ya Kasindaga, Katete, Kinesi (Karagwe), Nyakerera, Kyobuheke na Misambya na kwingineko, ambako Wanyarwanda wamejikatia mabuloku makubwa sana (Blocks) ambayo wazawa hawaruhusiwi kukanyaga, na wakithubutu ni kuuawa. Kitendo cha Kagame na Museveni cha kuifanya Nchi yetu kwamba haina Utaifa na heshima ya mipaka yake ( sovereignty and territorial integrity) kama zilivyo nchi zao, ni Tangazo la Vita! Ni lazima tujibu mapigo kwa nguvu kuliko tulivyomjibu dikteta Idd Amin Dadah. Majeshi yetu yaanze mazoezi makali ya vita, na raia waanze upya mafunzo ya mgambo kwa ajili ya Nchi yetu. Kama lilivyoanza tatizo la uvamizi wa Kagame DRC Mashariki, maelfu ya Wanyarwanda tayari wamekamata ardhi yetu kubwa sana, kwa kutumia vibali bandia vya kuishi nchini, na makaratasi ya uraia bandia wa Nchi yetu. Jasusi la Kagame liitwalo Athanas Kafurama mara nyingi hudhalilisha wazawa wa nchi yetu kwamba hawana kitu vichwani, na kwamba Tanzania inamjali mtu mwenye pesa yaani kama wao, na siyo raia wake walalahoi! Kagame amefanikiwa kwa sehemu kubwa kuiteka kimya kimya mikoa yetu ya Kagera na Kigoma! Hata Mkuu wa Mkoa wa Kagera Col. Fabian Masawe unamwuma moyo, jinsi Kagame na Mseveni walivyopenyeza askari zaidi ya 35,000, waliojichimbia na maelfu ya ng’ombe, hasa katika Hifadhi ya Taifa ya Buligi. Wanyarwanda wamekamata ardhi yetu kubwa sana, bila kuwa hata na vibali vya kuwepo nchini mwetu.Kabla ya kueleza zaidi juu ya uvamizi wa Buligi mkoani Kagera, tunapenda ifahamike kwamba Mkoa wa Kigoma umeingiliwa na Wanyarwanda na Warundi zaidi ya 100,000, ambao tayari wameteka sehemu kubwa ya ardhi ya Taifa letu, katika upanuzi wa Himaya yao. Tena wanajipenyeza kupitia katika makanisa maalum yanayoeleweka. Tayari wameanza kufanikiwa kukamata utawala wa Nchi yetu, kama vile Mnyarwanda aitwaye Peter Serugamba alivyoteka Jimbo la Kigoma Mjini, au Diwani John wa Kata ya Gungu. Watusi wamegundulika kuwamwagia rushwa viongozi wa vijiji na vitongoji ambao wanawatumia kuiteka ardhi yetu, na nafasi hizo wamepanga kuzichukua wao katika kuijenga Himaya yao. Vikao vya Watusi vya mikakati yao ya kuitwaa Nchi yetu katika Himaya yao mjini Kigoma hufanyikia katika hoteli ya Coast View, iliyojengwa kwa mtaji uliotoka Rwanda, ambao ni utajiri ulioporwa Congo. Watusi hawafichi katika majigambo yao, kwamba wanaweza wasilazimike kutumia nguvu za kijeshi kuitwaa ardhi ya Tanzania, kwa sababu eti wanaweza kutumia rushwa tu na akili kuichukua yote bila shida! Wanaujua udhaifu wetu kwa sababu walijipenyeza katika ngazi zote za utawala wa Nchi yetu, katika majeshi yetu, Uhamiaji, Taasisi zetu za fedha, Usalama wa Taifa n.k. Ndiyo maana Nchi yetu takatifu imetumika katika unyama wa kutisha kwa maslahi ya Watusi. Ni kweli pia kwamba nchi yetu inao watawala wanaoweza kununuliwa kirahisi kwa mapesa ya Wanyarwanda, ng’ombe zao na au mabinti wa Kitusi. Ndiyo maana wanampigia debe na kumwinamia mwuaji wa kutisha Paul Kagame, wakati wanajua kabisa kwamba: 1. Kagame amemwaga kinyama sana damu ya mamilioni ya Wahutu, ambao bado anaendelea kuwaua usiku na mchana, kuliko Adolf Hitler alivyowaua Wayahudi. 2. Kagame anaendesha mauaji dunia nzima, kwa kutumia kikosi chake maalum cha Escadron de la mort, ambacho ndicho alichotumia hata kumwangamiza Bingwa wetu wa Sheria, Hayati Profesa Jwani Mwaikusa, kwa kosa la kuweka wazi katika ICTR kwamba mtuhumiwa mkuu wa genocide katika Maziwa Makuu ni dikteta Paul Kagame. Kagame alihofia kwamba kutokana na majumuisho ya mwisho ya Mwanasheria huyo, lazima Ulimwengu ungelazimisha kukamatwa kwake na kufikishwa mbele ya Sheria. 3. Kagame akiwa na cheo cha Meja alikuwa mstari wa mbele kumwua Rais Thomas Sankara wa Burkina Faso, kule Uagadougou. 4. Kagame alikuwa Burundi kwa ushirikiano wake muhimu na Jean Bikomagu, katika mauaji ya kikatili sana ya marehemu Rais Melchior Ndadaye. 5. Kagame ndiye aliyehusika kikamilifu na utunguaji wa ndege iliyomchukua Rais Juvenal Habyarimana wa Rwanda pamoja na Rais Cyprien Ntaryamira wa Burundi. 6. Kagame analaaniwa na dunia nzima kwa kumfanyia unyama wa kutisha mwanasiasa mwanamke, shujaa Victoire Ingabire, ambaye amemtupa gerezani kwa kosa la kugombea Urais wa Rwanda akiwa Mhutu, na kosa la kuwa na kibali kwa wananchi wa Rwanda kuliko yeye aliyeloa damu ya mamilioni ya binadamu aliowaua kinyama. 7. Kagame amemwaga majasusi zaidi ya 1,000 katika Nchi yetu, wanaotumia ufisadi wa mapesa, ngono n.k katika kutengeneza mazingira ya kutekwa utawala wa nchi yetu na Watusi na hatimaye nchi yetu kuwa mkoa wa Himaya yao. Kama ilivyoelezwa juu, maelfu yao wamefanikiwa kujipenyeza katika taasisi zote nyeti za dola ya Nchi yetu. Walipoishika Uhamiaji waliitumia kujipa uraia na kukamata nafasi nyeti na ardhi yetu pia. 8. Maelfu ya majasusi wa Kagame wanajifanya wanashughulikia mizigo ya Rwanda na Uganda, wengine wanajifanya wafanyabiashara au wanatafuta kuwekeza, wengine wanajifanya wanafunzi. Lakini ukweli ni kwamba Taifa letu liko uchi kwa Kagame, kwa sababu kila tunachokifanya katika Nchi yetu kinaripotiwa Rwanda masaa 24. Katika Jiji la Dar es Salaam, Mikocheni ndiko walikojaa Wanyarwanda hao kama kwao. ANGALIZO: Jumuiya ya Afrika Mashariki ilivunjika mwaka 1977 kwa sababu moja tu kwamba ilishindikana viongozi wa nchi tatu wananchama yaani Tanzania, Kenya na Uganda kukutana pamoja, kwa ajili ya kupitisha maamuzi yote muhimu ya uendeshaji wa shughuli zote za Jumuiya. Kwa sababu Rais Julius Nyerere alikataa kukaa meza moja na Rais Idd Amin Dadah wa Uganda, kwa sababu Amin alikuwa mwuaji. “Siwezi kuchangia meza moja na mwuaji aliyeloa damu” alitamka Rais Nyerere, ulimwengu wote ukamuunga mkono hata mgomo wake uliposababisha kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki! SWALI: Ikiwa Nyerere alikataa kukaa meza moja na dikteta Idd Amin kwavile aliua binadamu takriban 350,000, Jumuiya ya Afrika Mashariki ikavunjika kwa sababu ya kuthamini uhai wa binadamu kuliko vitu vingine vyote, hawa watawala wetu wa leo wa CCM ni binadamu wa jinsi gani, ikiwa wanaweza kulikumbatia na kulipigia debe na hata magoti liuaji la kutisha kama Paul Kagame, lililoua kinyama binadamu zaidi ya 6,000,000 Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Tanzania, Kenya, na kuwapelekea wengine kifo kule kule Ulaya walikokuwa wamekimbizia uhai wao? Watu wa hatari kuliko wote kuhusu amani katika Maziwa Makuu ni hawa madikteta, Paul Kagame na Yoweri Museveni, walioangamiza mamilioni ya raia wa Maziwa Makuu, wakavamia Jamhuri dada za Rwanda na Zaire (DRC) na kuangusha tawala za mataifa hayo huru, na kuipora Congo mpaka dunia nzima inawapigia mayowe kama majambazi ya hatari! Watawala wetu wanakuwa katika akili za namna gani wanapokwenda Kampala na Kigali, na kukaa na Kagame na Museveni na kuzungumzia eti amani katika eneo la Maziwa Makuu, wakati hao ndio wavunjaji makatili wa hiyo amani? Hivi ni kweli akina Kikwete hawana hofu kwa Mwenyezi Mungu, kiasi cha kuamua kumsaliti jirani mwema aliyevamiwa na kuangamiziwa mamilioni ya raia wake kwa kosa tu la kuwa Wahutu, na kuwasaidia maharamia waliomvamia? Ni aibu kubwa zaidi kwamba watawala wetu waliishia kukubali umamluki, wa kuwasaidia Kagame na Museveni majeshi eti yakawasaidie kuangamizia Wahutu waliopokonywa nchi yao ya Rwanda, na mashujaa wanaopinga udikteta wa damu wa Yoweri Museveni nchini Uganda! Huku ndiko kuhimiza kisasi cha Mwenyezi Mungu juu ya nchi yetu!
Posted on: Thu, 08 Aug 2013 09:16:56 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015