KARIBU UNAWEZA KUTOA MAONI KATIKA TAARIFA YA HABARI YA BOMBA - TopicsExpress



          

KARIBU UNAWEZA KUTOA MAONI KATIKA TAARIFA YA HABARI YA BOMBA FM-MBEYA ya SAA 10;00 JIONI HII, MIONGONI MWA HABARI ZETU>>> 1. Wananchi wa kijiji cha Mwambani wilaya ya Chunya mkoa wa Mbeya wamegoma kuuzika mwili wa MAGAKA TINYA aliyefariki dunia September 24 baada ya kugongwa na gari la halmashauri ya wilaya ya Chunya wakati wa zoezi la kuwaondoa wafugaji katika eneo oevu. 2. Mwenyekiti wa tume ya katiba Tanzania Jaji Mstaafu JOSEPH WARIOBA amesema kuwa tume yake imeanza kukaa kama kamati kwa lengo la kujadili na kuchambua maoni yaliyotokana na mabaraza ya katiba hapa nchini. 3. Baadhi ya wakazi jijini Mbeya wameonekana kuingiwa na hofu ya uvamizi dhidi ya makundi ya kigaidi zikiwa zimepita siku chache tangu wanamgambo wa alshababu kuvamia jengo la Westgate nchini Kenya. 4. Zaidi ya vocha 43,000 zimekwisha sambazwa kwa wakulima wa wilaya za Ileje, Rungwe na Mbeya kutokana na kuwahi kwa msimu wa kilimo katika maeneo hayo. 5. Tanzania leo inaungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya utalii ambayo kitaifa itafanyika mkoani Mwanza. NA 6. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupiga kura kupitisha azimio la kutaka kuangamizwa kwa silaha za kemikali zinazomilikiwa na serikali ya Syria. MSOMAJI:- GREYSON SALUFU. Bofya hapa kusikiliza redio online ustream.tv/channel/bomba-fm-radio-online.
Posted on: Fri, 27 Sep 2013 12:53:52 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015