KUOTA UNAKIMBIZWA NA NYOKA : ni ujumbe kwako kwamba roho ya uongo - TopicsExpress



          

KUOTA UNAKIMBIZWA NA NYOKA : ni ujumbe kwako kwamba roho ya uongo inakunyemelea maana nyoka katika ulimwengu wa roho ni roho ya uongo na kumbuka shetani alivaa umbo la nyoka na kuwadanganya hata akina Adamu na Hawa katika bustani ya edeni wakatenda dhambi (Mwanzo 3:4) na katika Ufunuo 20:2 shetani anaitwa nyoka wa zamani yaani aliyewadanganya akina Adamu na Hawa. Hivyo ni kuwa makini sana na kuvunja roho hiyo kwa jina la YESU KRISTO na mpango huo wa kuzimu hautafanikiwa. Na mfano mzuri ni mimi siku moja nikiwa kanisani tunaomba nilimwona nyoka anazunguka na kwa sababu nilikua sijajua kwamba hiyo ni roho ya uongo unanyemelea watu wa MUNGU hakika kesho yake ulizuka uongo mkubwa na kusababisha hadi baadhi ya viongozi wa kanisa kukosana na ndio ikawa mwanzo wa mimi kujua kwamba nyoka anamaanisha nini katika ulimwengu wa roho. MUNGU akubariki sana ndugu na kumbuka kuwa suluhisho pekee la yote haya na yote yanayowasumbua wanadamu ni YESU KRISTO na yeye mwenyewe katika Mathayo 11:28
Posted on: Sat, 29 Jun 2013 11:41:30 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015