KWA GIA HII…MAENDELEO YETU NI KAMA MAYAI YA POPO!!! Najivunia - TopicsExpress



          

KWA GIA HII…MAENDELEO YETU NI KAMA MAYAI YA POPO!!! Najivunia sana kuwa Mtanzania, tena mtanzania mzalendo! Napenda sana maendeleo ya nchi yangu na nafurahia sana juhudi za kweli za serikali za kuleta maendeleo; Najivunia viongozi wanajitoa kwa moyo moyo wote kutimiza majukumu yao ya kila siku, najua ni wachache sana ukilinganisha na wengi ambao wameacha kabisa madili yao ya kazi,wameacha kutumia vichwa vyao ila sasa wanafikiri kwa kutumia tumbo. Maisha ya mtanzania wa kawaida ni magumu,tena sana,lakini bado hawaachi kuipenda nchi yao naam hata pamaoja na utitiri wa kodi na michango bado watu wanatoa tu bila hiana. Ugumu wa maisha ndio unaongeza uhalifu,ujambazi,umalaya na hata uuzaji wa dawa za kulevya,bado naamini serikali inaweza kushughulika kwa umakini mambo haya yote. Kila mwaka serikali imekuwa ikiongeza na kupunguza viwango vya kodi katika maeneo mbalimbali, na imekuwa ni utaratibu kwasasa kuwa kila mwaka lazima kodi ya Viburudisho pamoja na sigara ipande kitu ambacho kinafanya bei ya vitu ambavyo kodi yake inapanda kila siku kupanda sana….serikali huwa inakuwa ina majibu mepesi tu kwa hata maswali magumu. Yaani nakuwa mashakani kuhoji na kutafakari uwezo wao wa kufikiri na ubunifu wa kutafuta vyanzo vipya vya mapato kama uko sawasawa. Maana serikali kila kukicha inaongeza matumizi lakini haitafuti vyanzo vipya vya mapato vya kueleweka…kwanza serikali yenyewe ni kubwa mno, wizara nyingi sana, maofisa wa serikali ni wengi sana wanaotumia magari ya ghali sana kuyanunua na hata kuyahudumia, safari nyingi sisizo za msingi,safari ambazo hazina matunda zaidi ya kufuja tu,misafara mirefu ya viongozi wa serikali na bado serikali inaendelea kuongeza idadi ya mikoa na wilaya na kuwa na vipao mbele dhaifu,uthibiti hafifu wa fedha za serikali na hata kama watu wakigundulika wameharibu bado wanalelewa mpaka tunasahau….SASA HAMNA NAMNA TUNAWEZA KUENDELEA KWA KUTUMIA ZAIDI YA KUZALISHA. CHANZO KIPYA CHA KODI KIMEBUNIWA; Mwaka huu wa fedha serikali imeongeza kodi kadhaa ikiwepo kodi ya mafuta ya taa na mawasiliano ya simu za mkononi,kitu ambacho kinaleta maumivu kwa watu wa chini kabisa….na hiyo hasara sio ya mitandao ya simu,maana na wao wameongeza gharama za mawasiliano…..zaidi eti wamebuni chanzo kipya cha mapato….”TOZO ZA KILA MWEZI KWA KILA KADI YA SIMU”…..Katika hili naona wanastahili pongezi (ikiwa uwezo wao wa kufikiri umeishia hapo),lakini siwezi kuunga mkono hata kidogo ikiwa tunaweza kufikiri kwa kina na kupata vyanzo vipya vya mapato. KODI NYINGI MNO MKONONI MWA MLALA HOI; Haiwezekani huyu mtumiaji wa simu alipie kodi muda wa maongezi,maongezi yenyewe,huduma za kibenki za simu, huduma nyinginezo kama vile za mwito kwa akupiaye,habari na nyinginezo ambazo kuna wengi wameunganishwa na wameshindwa kujitoa hata sasa……NA SASA TUNATAKA MTU AANZE KULIPIA KADI YAKE YA SIMU KILA MWEZI….hapana huu ni uonevu. Hivi hamuwezi kuona ni jinsi gani makampuni haya ya simu mmeyaachia pesa nyingi sana? kwanza hayasemi ukweli kuhusu uwekezaji wao na faida wanayoipata hapa nchini kwetu na hakuna ufuatiliaji wa kweli(monitoring) wa serikali…yaani mambo yanaendeshwa kienyeji tu….ujio wa huduma za kibenki kwenye simu za mkononi umeleta changamoto sana kwenye biashara ya mabenki,hususani mabenki yanajishungulisha na watu wa kawaida,zikiwemo hata zile zenye hisa za serikali. NI VEMA KUJUA NA HAYA PIA; Watu wanaojishulisha na uwakala wa huduma za kibenki za simu za mkononi,wanaweza kuwa wanapata faida lakini haifanani na hatari inayowakabili,maana hawana bima ya kazi hiyo….ukiwa na sehemu yako unapofanya uwakala,ikitokea majambazi wamekuvamia na kuchukua pesa zote,hiyo sio hasara ya kampuni ya simu bali wewe mwenyewe….na zaidi watu tunaoweka fedha huko,hatuna hakika saaana maana siku wakiamua kufuta kumbukumbu kwenye DATABASE yao basi tena,kwani utadai wapi?,utaenda mahakama gani na utathibitishaje kuwa ulikuwa na Milioni kwenye simu?…Kama hili ni gumu basi sawa,naamini wengi hawajapona na maumivu ya DECI hata sasa. Ieleweke kuwa sijasema hawa jamaa ni matapeli hapana,ila natamani serikali ione namna nyingine ya kufuatilia kwa karibu mambo haya…itafaa sana kama mihamala yote ingekuwa inaonekana TCRA moja kwa moja…hapo kodi na usalama fedha ungekuwa ni wa hakika,LAKINI KWA KUWA TUMEAMUA HIVYO HAMNA NENO. VYANZO VINGINE VYA KODI; Kuna vyanzo vingi sana vya kodi,ambavyo vikipangiliwa basi tutakuwa mbali sana,ngoja nitaje vichache tu; 1. Kwenye mipaka mingi ya nchi hii biashara ya kubadilisha fedha inafanyika kiholela tu,kwa hiyo hakuna kitu serkali inapata,maana watu hawa wanafanya biashara na fedha mkononi….mfano mzuri ni Tunduma,mpaka wa Zambia,DRC na nchi zote za kusini,ikiwepo na Afrika kusini….je ni kiasi cha kodi inapotea hapo na mipaka mingine? 2. Wajenzi/vibarua wa ujenzi waliotapakaa nchi nzima..inawezekana serikali inachukua kodi kwa makampuni ya ujenzi peke yake,lakini asilimia 90% ya nyumba za nchi hii zinajengwa na mafundi wa kawaida…na hawa hawatambuliki popote na wala hawalipi kodi yoyote…kama serikali ingeona ni namna gani inawatambua na kupata kodi kwako,naamini inatosha sana kuongeza mapato ya serikali. 3. Wapangishaji wa nyumba, maduka na fremu mbalimbali za biashara…hii ni nchi pekee ambayo hakuna uthibiti kabisa katika eneo hilo,yaani kila anajipangia kodi atakayo na kila mwaka inapanda kwa ushawishi wa madalali,tena eti wanataka kodi ya mwaka mzima…kwanini serikali haioni kama hapa pia kuna kodi? kama ukiwekwa utaratibu unaoeleweka wa wapangishaji kulipa kodi pamoja na madalali,naamini pia ni chanzo cha uhakika kabisa cha kodi. 4. Kazi za Sanaa…ingawa serikali inaleta mpango wa kuweka stika za kodi kwa kazi za sanaa,lakini bado naona hakuna mkazo sana maana imewekwa kama hiari ya msanii mwenye kazi hiyo,lakini laiti ikiwa ni sheria kuwa kila CD/DVD ama kazi yeyote ya sanaa ilipe kodi,pamoja na hizi filamu toka nje ya nchi,hususani hizi filamu zinazokuwa nyingi ndani ya moja ,nina uhakika Sanaa ya ndani ingeheshimika,wasanii wangeneemeka na serikali ingepata mapato ya kutosha. HIVI NI VICHACHE TU KATI YA VILE AMBAVYO SERIKALI INAWEZA KUVIFIKIA NA KUVIFANYIA KAZI,LAKINI ZAIDI KAMA SERIKALI INGESIKILIZA KILIO CHA WATANZANIA CHA MUDA MREFU CHA KUREKEBISHA KODI KWA MAKAMPUNI YA MUCHIMBA MADINI PAMOJA KURUDISHA KODI MBALIMBALI ZILIZOFUTWA,IKIWEMO KODI YA UINGIZAJI WA VIPURI NA MAKEMIKALI YA KUCHIMBIA MADINI; KODI ZA MAKAMPUNI YA UTALII NA MAHOTELI, NINAAMINI SERIKALI ITAKUWA NA FEDHA NYINGI SANA ZA KUTUMIA. USHAURI WANGU KWA SERIKALI; 1. Lazima itafute timu ya watu wanaoweza kufikiri na kubuni vyanzo vipya vya mapato kwa faida ya kesho ya Tanzania 2. Serikali ipunguze matumizi ya kawaida na kuongeza uwekezaji wa ndani; fedha ifanye maendeleo sio iishe kwa matumizi ya kawaida na mishahara. 3. Serikali iongeze uthibiti wa mapato hayo yanayopatikana hata kama ni kidogo,maana haina maana kuwatesa wananchi na bado serikali inawafuga mchwa wanaotafuna na kufuja pesa za walipa kodi. 4. Serikali lazima iwapende wanachi wake,kwa kuweka kodi kubwa sana vitu kutoka nje kuingia ndani na hayo makampuni makubwa ya uwekezaji na kupunguza mzigo wa kodi wa wananchi wa kawaida….zaidi serikali iache dharau,haiwezekani JKT watengeneze fanicha lakini yenyewe iagize fanicha za serikali nje ya nchi. 5. Ipunguze matumizi yasiyo ya lazima kwa kutoa mitaji kwa baadhi ya taasisi zake ili zijiendeshe zenyewe….mimi ninaamini JKT na MAGEREZA vinaweza kujiendesha na kujitosheleza kama wakiwepo watu makini na kama serikali ikijidhatiti kweli. MWISHO; Binafsi bado ninaamini kuwa ipo nafasi ya kujirekebisha, haiwezekani nchi hii iendeshwe kwa “DHARULA” katika kila eneo…yaani Umeme dharula,Elimu Dharula,sasa imekuwa ni kama utaratibu vile,haiwezekani kukurupuka tu katika kila jambo…mambo mengi kwenye nchi hii yanaenda kama vile hamna wasomi ati,Wakati amekuja Obama ndio niligundua uzembe mwingi sana,lakini leo sisemi lolote hapa,ila lazima ijulikane kuwa Wazalendo bado tupo wengi sana na tunaamini serikali inasikia maoni ya wananchi bila hila,hivyo kwa niaba ya wanachi naomba na yangu myafanyie kazi….Msione wananchi wana line mbili na kuendelea mkadhani labda maisha ni mazuri sana,hapana,ni kuwa mtu anajaribu kupunguza gharama kwa kupiga watu wa mtandao huu kwa kadi husika na ule vile vile. Wasomi nchi hii bado hawajaheshika wala kutumiwa vema. Pamoja na yote yanayoendelea katika nchi, bado ninaipenda nchi yangu na kamwe sitoacha kuipenda maana nilizaliwa hapa kwa kusudi maalum,naam mpaka kusudi hilo litakapotimilika ndio nami nitapumzika katika maisha haya. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA NA WATU WAKE WOTE, AMEN! Na. CHAVALA, FREDY E. +255 713 88 37 97 tanabaisho.wordpress tanabaisho.wordpress/2013/08/05/130/
Posted on: Mon, 05 Aug 2013 12:23:51 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015