Kawaida mwenye kukemea ni yule ambaye atajua kuwa hilo ni kosa na - TopicsExpress



          

Kawaida mwenye kukemea ni yule ambaye atajua kuwa hilo ni kosa na yule ambaye haweki maslaha yake ya kidunia na tumbo mbele. Ama yule aliyezoea kulifanya na kulishiriki, basi si rahisi kulikemea, ingawa wengine pembeni huwa wanakiri na kusema: “Unajua twende na watu watakavyo, au jamii ilivyozoea, tukipinga yaliyozoeleka tutakosa uluwa na hatutakubalika wala kusikilizwa”!! Kwa hiyo jambo hilo la kisomo cha Arubaini na kufanyiwa chakula halimo katika sheria na halipasi kutendwa kwani ni bid’ah iliyokemewa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na akatuhidhirishia madhara yake kuwa ni upotovu na adhabu zake ni kujitayarishia makazi motoni. Na Allaah Anajua zaidi
Posted on: Sat, 19 Oct 2013 21:02:52 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015