Kizazi cha sasa kina haki ya kuelewa ni jinsi gani muungano huo - TopicsExpress



          

Kizazi cha sasa kina haki ya kuelewa ni jinsi gani muungano huo ulivyoanza na malengo yake yalikuwa yapi. Hiyo ni haki ya kila mtu katika nchi hii inayoitwa Tanzania. Inawezekana, na ni dhahiri huko nyuma, hususani wakati wa utawala wa Nyerere, watu wengi walikuwa waoga kuhoji muundo na uhalali wa muungano huo. Lakini, woga wa wananchi haukufanya kasoro za muungano ziondoke. Ziliendelea kuwepo na viongozi waliofuata (baada ya Nyerere) wakajkinufaisha na woga wa Watanzania wengi waliokuwa wamefumba midomo yao. Lakini, ukweli huwa haufi au hauuawi! Wenye kuuhoji uhalali wa muungano huu bado wapo na kama kuna kasoro zilizokuwepo, bado zipo! Vilevile, wenye madaraka ya kuweza kuziondoa kasoro hizo bado wapo. Na wenye madaraka wasiotaka kuziondoa kasoro hizo, bado wapo pia! Kama nilivyosema, ukweli hauwezi kuuawa na nguvu yoyote duniani! Si kwa mazingaombwe wala risasi! Kama kweli muungano huu una kasoro za kweli, basi zitaendelea kuwepo daima, na asiyetaka kuziondoa kiungwana leo, ajue zitakuja kuondolewa kihuni na waungwana lakini kwa madhumuni ya kiungwana! Kukubali kosa au dosari ni ujasiri na huonyesha busara kwa mhusika kwani jamii hutambua kwamba mhusika ana uwezo wa kutambua jema na baya. Lakini, kwa mwenye kutaka kulinda heshima yake tu, ajue hubomoa si jamii tu, bali na heshima yake! Kama nilivyosema, kwa upande wa Bara, kura hiyo siyo ya lazima kwani hakuna sababu yoyote ya msingi ya kuwauliza watu wa Bara, kwani hawana hisia za kupoteza chochote kihistoria, kiuchumi hata kiutamaduni. Tatizo kubwa limekuwa ni kwa Wanzanzibari ambao daima wamekuwa na wasiwasi wa kumezwa kwa taifa lao na hivyo kupoteza historia na utamaduni wao ambao umekuwepo kwa karne nyingi. Kwa watu wenye msimamo wa busara na wasiojihusisha na upande wowote katika suala la muungano, watagundua kabisa kwamba madai ya watu wa Visiwani yaliyosababisha hadi kupata bendera yao, wimbo wao wa taifa, rais wao, katiba yao, na kadhalika, ni hatua za mwanzo za kutaka kuwa na nchi yao kamili inayotambulika duniani na katika taasisi zote ambazo nchi kamili hushiriki chini ya kivuli chake na si chini ya kivuli cha nchi nyingine.
Posted on: Fri, 02 Aug 2013 07:38:19 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015