Kulikuwa na tangazo la kazi, watu watatu, mwanafuzi, mhasibu na - TopicsExpress



          

Kulikuwa na tangazo la kazi, watu watatu, mwanafuzi, mhasibu na mwanasiasa wakapeleka maombi, siku ya usaili wakafika tayari kwa usaili; MSAILI: Je 2+2 ni ngapi? MWANAFUNZI: 4 MSAILI: Haya nenda niitie mwenzio MSAILI: Je, 2+2 ni ngapi? MHASIBU: Kwa ujumla ni 4, inaweza ikazidi kidogo au kupungua kidogo kwa asilimia kama 10 hivi lakini ni 4 MSAILI: Duh haya nenda niitie mwenzio MSAILI: Je 2+2 ni ngapi? MWANASIASA: Kitu kikubwa hapa ni kuangalia trend ya wapiga kura, haya mambo unaweza ukajibu kwa harakaharaka ukakuta mambo yamebadilika yakakukosti kwenye uchaguzi. Kimsingi kwanza ni muhimu kujua msimamo NA muelekeo wa Chama chako, na pia kuangalia je jibu lako lina matokeo gani katika muktadha mzima wa swala lenyewe. MSAILI: Hebu jibu swali 2+2 ni ngapi? MWANASIASA:(Kwa sauti ya chini) We unataka iwe ngapi bosi?
Posted on: Mon, 26 Aug 2013 12:23:07 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015