Laana zingine mnajitakia,mkeo /mchumba ndo alarm yako anakuamsha - TopicsExpress



          

Laana zingine mnajitakia,mkeo /mchumba ndo alarm yako anakuamsha asubuhi na mapema,ameshaandaa nguo mpka kifungua kinywa,ameweka viatu mlangoni ili ukitoka asipate shida ukachelewa kazini,unamwacha na majukum kibao ya kulea watoto na kuhakikisha unarudi kila kitu kipo sawa ona unavyomlipa mwisho wa mwezi ukifika. Unapanga mshahara wako ukampelekee kimada nusu ya mshahara unalipa madeni ya bia ulizokunywa na uliobali unapanga ni sh ngapi utatumia kunywea na marafiki na shoping za kimada wako kisha chench unampelekea mkeo nyumbani kwa ajili ya matumizi hata yeboyebo ya alfu mbili imekushinda kununua umpelekee kama asante. Halafu unalalamika una miaka mingi kazini huoni unachofanya hio ni laana mungu anaona kimada umemnunulia cm kali tatu anabadilisha atakavyo mkeo ana nokia ya tochi tena ameifunga na mnati maana imechakaa jaman kha! Mwogopeni mungu
Posted on: Mon, 29 Jul 2013 04:14:34 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015