MALKIA wa mipasho Khadija Kopa amepata pigo kubwa baada ya kufiwa - TopicsExpress



          

MALKIA wa mipasho Khadija Kopa amepata pigo kubwa baada ya kufiwa na mumewe usiku wa kuamkia leo. Mumewe huyo Jafar Ali ambaye pia ni Diwani wa kata ya Magomeni Bagamoyo amefariki katika hospitali ya Lugalo alikokuwa amelazwa kwa siku tatu. Khadija Kopa aliyekuwa Sumbawanga kwa shughuli za kikazi, yuko njiani kurejea jijini ambapo atatumia ndege ya Makamu wa Rais hadi Arusha na hapo itabidi achukue ndege nyingine hadi Dar es Salaam. Jafar Ali pia ndio alikuwa meneja wa Khadija Kopa. Mwili wa marehemu tayari umeondolewa hospitalini hapo na kupelekwa Bagamoyo. Taarifa za mazishi bado hazijatolewa saluti5/item/572-pigo-kubwa-kwa-khadija-kopa-mumuwe-afariki-dunia
Posted on: Thu, 06 Jun 2013 17:21:01 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015