MAREKANI imeitaka Rwanda kuacha kusaidia waasi wa kundi la M23 - TopicsExpress



          

MAREKANI imeitaka Rwanda kuacha kusaidia waasi wa kundi la M23 ambalo linaendesha mapambano dhidi ya Serikali ya nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Taifa hilo kubwa duniani limesema lina ushahidi wa kutosha kuonesha kuwa Rwanda inalisaidia kijeshi kundi hilo la waasi na baadhi ya maofisa wake wamo. Hii ni mara ya kwanza kwa Marekani kutoa kauli kali tangu kundi hilo lianzishe mapigano dhidi ya Serikali ya DRC katika mji wa Goma ulioko eneo la Mashariki, ambalo lina utajiri mkubwa wa madini.
Posted on: Thu, 25 Jul 2013 02:38:53 +0000

© 2015