MFICHA UCHI HAZAI. Mfumo mpya wa utahini wa mitihani ya kidato - TopicsExpress



          

MFICHA UCHI HAZAI. Mfumo mpya wa utahini wa mitihani ya kidato cha nne na cha sita unaweza kugeuka kuwa majanga kama hapatakuwa na nguvu kazi ya kufuatilia ukweli wa maendeleo ya kila mwanafunzi alipokuwa shuleni. Kwa hali ilivyo, watoto wengi wanaweza kupewa alama nyingi sana na shule zao katika mitihani ya ndani ya shule na kanda na wakaonekana wamefaulu sana. Mtihani wa mwisho ukifika ndo mtoto anapata alama za chini na mzazi anashangaa. Ili kuboresha elimu katika nchi yetu; 1. Tuwe na madarasa ya kutosha na ya uhakika, 2. Tuwe na vifaa vya kufundishia na zana zote muhimu za mafunzo ya vitendo darasani na nje ya darasa kwa walimu na wanafunzi, 3. Tuwe na walimu wa kutosha na wenye ujuzi wa kuridhisha, 4. Tuwape walimu wetu mishahara na maslahi mazuri(tusifikiri kuongeza mishahara kwa wabunge na wakubwa serikalini hadi sasa imewakinai), 5. Hebu tuhakikishe walau zaidi ya nusu au robo tatu ya walimu wa shule zetu zote wanaishi katika nyumba za kisasa na zilizo karibu na shule wanazofundisha. 6. Tuweke mazingira ya uhakika kwa wanafunzi wetu kuhudhuria shule na wazazi na walimu washirikiane kuhakikisha hili. Tukifanya haya na mengine mengi tutazalisha vijana wenye elimu iliyopevua fikra pana zinazoweza kupeleka elimu mbele. Binafsi sikubaliana kabisa na hii mbinu ya kushusha alama za ufaulu, kufuta daraja sifuri n.k.. Hizi ni hatua za kuzunguka mbuyu tu na ni za kujidanganya na kutudanganya sote. Kuna sababu zinazofanya vijana wanafeli mitihani na hawafanyi vizuri na wanakuwa na uelewa mdogo wa kimasomo. Sababu hizi hazitaondolewa na kushusha alama za ufaulu, zitaondoka ikiwa serikali itakubali udhaifu uliopo katika mfumo wa elimu na kukubali kukaa chini na wadau wote muhimu kupata masuluhisho muhimu ya pamoja. Tanzania tunayoitaka imo mikononi mwetu, tusifikiri haya watakuja kufanya wazungu, ni sisi wenyewe.
Posted on: Fri, 01 Nov 2013 10:41:55 +0000

Trending Topics



verdade-está-uma-topic-1424775404400544">prá quem acha que os crentes não pregam a verdade! está uma
Victor Borg When faced with lays offs Lawrence Gonzi and Tonio
Buy Compaq Presario CQ60-220US 15 6-Inch Laptop On Black Friday &

Recently Viewed Topics




© 2015