MISRI KUBADILISHA KATIBA YA KIISLAMU Rais wa Muda Misri - TopicsExpress



          

MISRI KUBADILISHA KATIBA YA KIISLAMU Rais wa Muda Misri dly Mahmoud Mansour (kushoto) na Mkuu wa Jeshi Jenerali Abdel Fattah al-Sisi Rais wa Muda Misri dly Mahmoud Mansour (kushoto) na Mkuu wa Jeshi Jenerali Abdel Fattah al-Sisi Rais wa muda Misri amebuni kamati ya wataalamu wa sheria ambao watapandekeza mabadiliko katika katiba ambayo inasema taifa hilo linapaswa kutawaliwa kwa misingi ya sheria za Kiislamu. Rais Adly Mohammoud Mansour Jumamosi aliteua kamatu ya wataalamu 10 ambao watapendekeza marekebisho katika katiba ya Kiislamu iliyoidhinishwa wakati wa utawala wa Mohammad Morsi aliyetimuliwa madarakani na jeshi mwanzoni mwa mwezi huu. Mursi na wafuasi wake walikuwa wakisisitiza kuhusu katiba ya Kiislamu kutokana na kuwa waliowengi nchini Misri ni Waislamu lakini wapinzani ambao sasa wako madarakani wamekuwa wakitaka katiba ya kisekula isiyozingatia Uislamu. Katiba ya mpya ya Misri iliidhinishwa Desemba 2012 na asilimia 64 ya wapiga kura. Miezi sita baada ya kuidhinishwa katiba hiyo jeshi la Misri lilimuondoa madarakani Mursi na kuwatia mbaroni wananchama waandamizi wa harakati ya Ikhwanul Mislimin. Kwingineko maafisa wa usalama Misri wamevamia ofisi za Cairo za kanali ya televisheni ya Al Alam ya Iran inayorusha matangazo kwa lugha ya Kiarabu. Aidha mkuu wa ofisi ya Al Alam mjini Cairo Ahmad al Sioufi ametiwa mbaroni. Maafisa hao wa usalama hawakutoa sababu ya kitendo chao. Tokea Mursi apinduliwe na jeshi, maafisa wa usalama nchini humo wamefunga stesheni kadhaa za televisheni katika kile kinachoonekana kuwa ni juhudi za kuzima sauti ya wapinzani.
Posted on: Sun, 28 Jul 2013 10:11:15 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015