MSAMAHA NDIO MSINGI WA IMANI NA AMANI. Nimeamua nitunge hii - TopicsExpress



          

MSAMAHA NDIO MSINGI WA IMANI NA AMANI. Nimeamua nitunge hii kaulimbiu toka ktk uvungu wa nafsi yangu lakin,kabla hatujaenda mbal zaidi,ni vema tukatambua maana halisi ya neno MSAMAHA.Kisha lazima tujue,nini maana ya suluhu,kwani msamaha na suluhu ni kama pande mbili za sarafu. Katika kitabu chake cha LEARNING TO FORGIVE,Doris Donelly analifafanua neno msamaha akisema,"forgiveness is a part of process which begins with hurts and ends_as its final and long ranged goal_with an event of reconciliation".Donelly anakwenda ndani zaidi kwa kusema,"forgiving is an extended,empowed and strengthened form of giving. According to Longman Dictionary of Contemporary English New edition,forgiving is to stop from being angry with someone and stop blaming them,although they have done something wrong.Pia katika maelezo toka kwenye kamusi hii,bado tunaona kuwa ktk mchakato mzima wa kusamehe kumbe lazima kuyasahau majeraha ya makosa ya watesi wetu kama anavyoeleza kuwa,"...although they have done something wrong". Kutoka katika maana halisi mbili_kumradh kwa kukosa rejea za kutosha_hapo juu,moja kwa moja tunapata jibu la kipi kitangulie,msamaha kwanza kisha suluhu,ama suluhu kwanza kisha msamaha? Kabla hatujaendelea,ni vema tukajiridhisha kwa kuangalia maana ya neno suluhu(reconciliation).Donelly,anasema,"...to reconcile means to rejoin two parts which belongs together but they are apart".Hivyo hapa moja kwa moja ni dhahiri kwamba,MSAMAHA kwanza halafu Suluhu ifuatie.Bado Donelly anakazia kwa kusema,"...people move swiftly from forgiveness to the reconciliation process without taking a stock of hurts".Kumbe ni lazima tuyaponye kwanza majeraha ya maumivu nafsin mwetu ili kutengeneza mazingira mazuri ya suluhu! Mfano mzuri ni pale mzazi anapojaribu kuwapatanisha wanae wawili wanaogombana,kuwalazimisha kushikana mikono ama kupigana busu-kama ishara ya upatanisho-si kitu endapo hawa watoto hawajasameana na kusahau chanzo cha maumivu yao.Nchi na nchi-kwa mfano Afrika ya Kati-zimekuwa zikikalishwa chini kwa ajili ya upatanisho,lakini vita vingi vimeripotiwa kuendelea mara baada tu ya mazungumzo haya.Sababu kubwa hapa ni kwamba,hakuna msamaha wa kweli baina ya nchi hizi ila ni upatanisho tu,na upatanisho bila msamaha ni sawa na kuchemsha sufuria tupu na kukaa pembeni ukisubiria supu. Kwa nini watu hushindwa kusamehe? Nini hutokea kwa mtu asiyesamehe? Ungana nami jumapili ijayo katika sehemu ya pili ya makala hii. Kwa ushauri,maoni na maswali ni-check kwa +255 759 947 397 au kwa barua pepe. sainthussein@gmail somo langu ni MSAMAHA NDIO MSINGI WA IMANI NA AMANI.
Posted on: Sat, 21 Sep 2013 22:57:07 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015