MUUNGANO WA CORD WAPINGA MRADI WA NYUMBA KUMI MUUNGANO wa Cord - TopicsExpress



          

MUUNGANO WA CORD WAPINGA MRADI WA NYUMBA KUMI MUUNGANO wa Cord umepinga vikali mpango wa Nyumba Kumi ulioanzishwa na Serikali kama mbinu ya kukabiliana na utovu wa usalama nchini. Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amesema wanashuku kuna njama inayopangwa kupitia mradi huo, kwani wananchi hawakuhusishwa katika uamuzi wa kuuanzisha. Odinga ambaye ni mmoja wa vinara watatu wa Cord aliongeza kutokana na kuwa pesa za umma zitatumiwa katika utekelezaji wa mpango huo, ingekuwa vyema iwapo wabunge wangehusishwa kuamua kiwango ambacho kitatumiwa. Alikuwa akiongea katika makao makuu ya ODM, Nairobi, baada ya mkutano wa wabunge na maseneta wa chama hicho. Kwenye taarifa ya pamoja iliyosomwa na Seneta Maalum Agnes Zani, Cord ilifananisha mpango huo kama utawala wa kipolisi, na kusema ni unaokiuka katiba. Na William Khaemba Mwanahabari K.U. 99.9 fm
Posted on: Tue, 19 Nov 2013 15:37:52 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015