Majanga:Ingekuwa wewe ungefanyaje Tirriika Ndugu zangu naombeni - TopicsExpress



          

Majanga:Ingekuwa wewe ungefanyaje Tirriika Ndugu zangu naombeni mnisaidie. Mwaka 2011 nilipata mchumba na sikufanya nae mapenzi kwa kuwa tokea mwaka 2004 nilivyotembea na wenye ukimwi 2 na kuona nipo salama niliamua kuachana na masuala ya kujamiiana. Nilivumilia mpaka ikafika mahali nikawa naona kawaida na wanawake wote nilikua naona ni dadazangu. Mwezi wa 2 mwaka huu nimemlipia mahali huyo mchumbaangu hasa baada ya kupima na kuona tupo salama wote na ndipo nilipoamua kuanza kujamiana nae. Wiki iliyopita alikuja kwa ajili ya kukamilisha masuala ya vifaa vya harusi na tulijamiina kweli si utani. Baada ya siku 2 tu nikaona hali si salama kwangu nikaamua kwenda kupima nikaonekana nina maambukizi ya GONO. Hivi nimemaliza juzi sindano 6 na nimemuuliza akakataa kabisa kwamba yeye hahusiki. Nimemshauri akapime kakataa kabisa. Nisaidieni ndugu zangu nifanyaje? Ndoa kanisani inatangazwa na maandalizi yote yameshaisha. Nashindwa kuelewa nifanyaje na kiukweli nimechanganyikiwa kabisa ndugu zangu. NISAIDIENI !!!
Posted on: Thu, 18 Jul 2013 09:24:27 +0000

Trending Topics




© 2015