Majangaaa Mbona Majangaaa! - 3- ILIPOISHIA “MAJANGAAA, jamani - TopicsExpress



          

Majangaaa Mbona Majangaaa! - 3- ILIPOISHIA “MAJANGAAA, jamani mbona Majangaaa!” alisema Eddy kimoyomoyo wakati alipotoka nje na kukutana na wasichana hao kibao wakiwa wamejipanga uwani kwa ajili ya kusubiri kwenda kuoga. “Samahani kaka naomba sabuni…” alisema yule msichana wa kwanza aliyewawahi wenzake kwenda msalani akimwambia Eddy. “Bila wasiwasi,” Eddy alisema na kumkabidhi binti huyo sabuni yake ya kuogea. “Daa! Unaanza kujipendekeza kwa mgeni,” alisema msichana mwingine na kuwafanya wengine nao waongeze maneno yao kedekede ambayo hata hivyo binti yule hakuyajali. NINI KILIENDELEA? POROMOKA NAYO… Baada ya muda binti yule alitoka bafuni na kwenda moja kwa moja kumrudishia Eddy sabuni yake, alipofika usawa wa chumba cha kijana huyo, Irene alikuwa na kusudio moja tu, kutaka kumshawishi ili awe wake hata kabla msichana yeyote anayeishi ndani ya nyumba hiyo hajamnasa. Alitaka kutumia ushawishi wake kumnasa mwanaume huyo ambaye alikuwa amemvutia kutokana na urefu wake na umbile lake la kimazoezi. Aliamini kabisa kwamba yeye ndiye aliyekuwa akiendana na mwanaume huyo tofauti na msichana mwingine aliyepanga pamoja na watoto wa baba mwenye nyumba. Tangu akiwa anamuomba sabuni, msichana huyo alikuwa ameshajua jinsi alivyoutega mtego wake wa kumnasa kijana huyo. Alitoka msalani akiwa amevaa kanga moja iliyokuwa ameilowanisha maji na kujaribu kujitingisha kwa mwendo wake wa madaha, moja kwa moja akawapita wasichana wengine waliokuwa wakigombea nafasi ya kwenda kuoga baada ya yeye kutoka. Alitembea kwa mwendo huo uliojaa uchokozi na kisha kuusogelea mlango wa chumba cha Eddy, bila ya kubisha hodi akaufungua kidogo na kuchungulia, wakati huo macho yake alikuwa ameyaachia kwa kuyalegeza na kuyafanya kama yatake kudondoka. “Kaka samahani sabuni yako hii…” alisema akiwa ameuingiza uso wake ndani ya chumba cha Eddy aliyekuwa akivaa kwa ajili ya kujiandaa kutoka. Eddy alishtuka na kumfanya binti huyo naye kujidai kumuomba radhi kwa kitendo alichokuwa amekifanya lakini wakati akifanya hivyo, tayari mwili wake wote ulishakuwa ndani ya chumba cha kijana huyo. “Naitwa Irene…” alisema huku akionekana kukikagua chumba kile kama vile alikuwa ametumwa kwa ajili ya kufanya kazi ya ukaguzi. Eddy alikohoa kidogo kutoa kikohozi kikavu kisha akamjibu: “Miye naitwa Eddy au Eddyson Manyara,” wakati huo kijana huyo alikuwa akichomekea shati lake. “Oooh oooh jina zuri sana… naona ndiyo unaanza maisha?” alisema Irene akiwa anamwangalia Eddy baada ya kukagua chumba hicho na kukiona kila kilichokuwemo ndani yake. “Eeehe, nimeamua kuondoka kwa wazazi na kuishi peke yangu ili kujipanga zaidi,” Eddy alisema kwa aibu. “Kwa hiyo umekuja kwa walimu tukufunze maisha?” “Sijakuelewa…?” alihoji Eddy. “ Siku zote Waswahili husema anayeshindwa na wazazi hufunzwa na walimwengu, siye ndiyo walimwengu wenyewe… karibu sana na jisikie kama uko nyumbani kwa wazazi wako.” “Aaah aaah…” Eddy alicheka na kuendelea kuvaa shati lake tayari kwa kutoka nje ya chumba chake na kwenda kwenye mihangaiko yake. “Unafanya kazi?” Irene alimuuliza Eddy. “Yaa, nafanya kazi…” “Sawasawa karibu sana…” alisema Irene huku akifungua mlango na kutoka nje kwa madaha, akijitahidi kuutingisha mwili wake. Wakati Irene akitoa mguu wake nje ya chumba hicho ghafla alipoinua uso wake kuangalia mbele akakutana uso kwa uso na Rehema akiwa anapita kwa ajili ya kwenda uwani. Rehema hakuonekana kumchangamkia Irene ambaye ndiyo kwanza walikuwa wakionana tangu kulipopambazuka siku hiyo. “Za asubuhi dada?” alisema Irene kumwamkia Rehema kwa haraka huku akichekacheka lakini salamu yake haikuitikiwa, akabaki ameduwaa. Rehema alimpiga jicho kali Irene kwa kumshusha na kumpandisha kisha akaenda zake uwani hali iliyomfanya Irene kufadhaika, moja kwa moja akajua kuwa ameingia kwenye vita na malkia wa nyumba hiyo. Irene alijaribu kufikiria ni nini kimetokea kati yake na Rehema lakini hakuambua kitu. Alifikiria labda jana yake alikuwa amemkosea, pia hakukumbuka kutokea kitu kama hicho. “Hivi huyu brother men anaweza kuwa chanzo?” alijiuliza akimfikiria Eddy. Nini kitaendelea? Usikose kufuatilia saa 8 mchana ............
Posted on: Thu, 15 Aug 2013 08:34:27 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015