Mpe Mpenzi wako sababu ya yeye kujilinda akiwa mwenyewe hata kama - TopicsExpress



          

Mpe Mpenzi wako sababu ya yeye kujilinda akiwa mwenyewe hata kama haupo...Usitumie Nguvu na Ubabe kumlinda kama hana sababu ya yeye kujilinda mwenyewe. Mpende na ajue anapendwa ili asiwe na sababu ya kuuchakachua upendo unaompa maana unamtosha kumlinda dhidi ya maupendo feki ya mtaani. Sasa wewe badala ya ku-invest muda wako kumpa Upendo wa kutosha,umejigeuza Alarm,unadhani kwamba unaweza kumlinda asiibiwe au asikusaliti...Unapoteza muda kumfuatilia anaenda wapi,na nani,na kwanini hajaaga,unamfuatilia nani kamtumia meseji na nani anaongea nae kwa simu mpaka unaenda kuprint statement kwenye mtandao anaotumia...Unapoteza muda wako Kama hujawahi kumiliki hata Shina la Mgomba utawezaje kumiliki mtu??? Mpenzi halindwi kama alarm,watu watai-Snooze na watamuiba kama kawa,Mpe sababu za kujiona anapendwa ili ajilinde mwenyewe.Kumlinda Mpenzi ni sawa na kulinda Bahari,wewe unalinda Coco Beach wenzio wanavua samaki Bagamoyo
Posted on: Thu, 26 Sep 2013 05:36:08 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015