Mwanamke amteketeza mjukuu baada ya kushuku si wa mwanawe POLISI - TopicsExpress



          

Mwanamke amteketeza mjukuu baada ya kushuku si wa mwanawe POLISI wilayani Butere wanamzuilia mwanamke wa umri wa miaka 60 aliyechoma mjukuu wake katika kijiji cha Emubia. Mshukiwa Alice Nanzai, anadaiwa kuchoma kibanda ambacho mjukuu wake wa mwaka mmoja unusu alikuwa akilala, na kuondoka hapo. Wanakijiji walisema alishuku kuwa, mjukuu huyo hakuwa mtoto halisi wa mwanawe wa kiume wake na alikuwa ameapa kumwangamiza. Mkuu wa polisi Butere, Bw Paul Wanjama, alithibitisha kisa hicho akisema mtoto huyo alichomeka kiasi cha kutotambulika. Kwa sasa, mshukiwa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Butere, nao mwili wa mtoto huyo ukiwa umepelekwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya misheni ya St Mary’s. Wiki chache zilizopita, mwanamke alimtupa mtoto wa siku moja kichakani kabla ya kitoto kuokolewa na msamaria mwema.
Posted on: Fri, 21 Jun 2013 08:00:31 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015