Mwanausalama Tanzania aaibika kutumia nguvu na mwanausalama wa - TopicsExpress



          

Mwanausalama Tanzania aaibika kutumia nguvu na mwanausalama wa Obama kumlinda mwandishi Mwandishi wa Gazeti Uhuru anayejulikana kwa jina Selina Wilson alienda makumbusho ambako kulikuwa na ugeni mzito wa Mke wa Obama Michelle Obama kwa mwenyeji wake Salma Kikwete. Selina alikuwa na kitambulisho kilichoonyesha kuruhusiwa Symbion, lakini jina lake lilikuwepo kwenye orodha ya pale Makumbusho. Kiongozi wa usalama Tanzania alimtilia nguvu mwandishi Selina Wilson na kumsukuma kwa nguvu atoke kwamba kitambulisho chake hakiruhusu kuingia pale ingawa jina lake lipo. Mwanausalama wa Marekani aliingilia kati na kumwambia mwanausalama wa Tanzania kosa la kitambulisho si hoja ya kumfukuza kwa nguvu kwa sababu jina lake limo kati ya waandishi wa habari walioruhusiwa kuwepo pale. Mwanausalama wa Marekani alienda mbali zaidi kwa kumwambia:"Ndivyo mnavyofundishwa katika utendaji wenu"? Mwanausalama huyo wa Obama alikasirishwa sana na kitendo kile cha udhalilishaji kilichofanywa na mwanausalama wa Tanzania, akaamua mwandishi Selina Wilson aingie kufanya kazi yake kwa vile jina lake lipo. Tukio hili ni la aibu sana kwa wanausalama wetu walivyo wanyanyasaji kwa wananchi na vyombo mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari nchini. Chanzo: habarileo.co.t
Posted on: Tue, 02 Jul 2013 08:07:45 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015