NDOA YANGU INANITESA Sahemu ya - TopicsExpress



          

NDOA YANGU INANITESA Sahemu ya #PILI #SIMULIZIII SIMULIZI TEL.0769-368 843 ILIPOISHIA Ulifika wakati baba na mama walitaka kuniachia laana baada ya kuwadanganya zaidi ya miaka kumi toka nipate pesa na kuwajengea nyumba. Walitaka wawaone wajukuu wao kabla ya kufariki, walijua umri walio kuwa nao,wasingeishi miaka mitano ama saba mbeleni wangepoteza maisha. Kwa kuwaridhisha na kukwepa radhi za wazazi niliwaomba wanitafutie Mke. SASA TUENDELEE Niliamini mke ambaye ningepewa na wazazi angenifaa maishani. “Baba akimpenda binti, hata mimi sina budi kumpenda” nilijisemea mwenyewe baada ya kuwapa kazi ya kunichagulia msichana mwenye sifa zote zile mwanamke anatakiwa kuwa nazo. Ni miongoni mwa nidhamu kwa mume. Nilikuwa na furaha kidogo, kwani nilijiona niliyejaa Ukungu wa kutopendwa na kutopenda. Kwa ujumla sikujua ilikuwa ni mitihani ya Mungu kwani mimi ni miongoni mwa vijana waliokuwa wakicheka vijana waliochaguliwa wachumba na wazazi wao, hakuna kitendo nilichokichukia kama kuchaguliwa msichana na wazazi. Nilikuwa na imani ya kijana akichaguliwa mke basi hata ndoa ingejaa migogoro isiyoisha na pengine ikavunjika. Kampuni yetu iliitwa JOPHU MINING TRANSPORT CO LTD, mwenye Kampuni yetu, alijulikana kwa jina la Mzee Jophu Kundy . Ndiye alikuwa Mkurugenzi na mmiliki wa Kampuni. Kipindi cha miaka ya sabini kulikuwa hakuna gonjwa la Ukimwi, kama lilikuwepo basi ilikuwa halijajulikana kama sasa. Nilikuwa nikienda Nchi Thailand kila wiki kuuza madini aina ya Tanzanite. Siku zote nilikuwa na urafiki wa karibu na mmiliki wetu Mzee Jophu. Hakuna hata mtu mmoja aliyethubutu kuongea na mzee Jophu aliyeonekana mwenye uso wa ukali saa zote. Haikuwahi kupita siku bila mzee Jophu kuita “Sweedy njoo” nk.Alikuwa kazoea jina langu , pia alinipenda kama mwanae. Siku moja niliondoka katika uwanja wa Kia (Kilimanjaro International Airport) nikielekea Nchini Thailand, Bang kok.Vaaa yangu toshani kielelezo kwa mtu asiyenifahamu,kusema mimi ni mtu mwenye pesa za kunifanya niitwe tajiri. Nilivaa suti ya kijivu,chini nilivalia viatu vya mchongoko,vijana wa sasa huviita ‘Mkuki moyoni’,mkono wa kushoto nilishikilia ‘breefcase’lililojaa madini ya Tanzanite.Pia nilivalia miwani ya jua,iliyosababisha vigumu kuona macho yangu. Nilikuwa nimebeba madini gram 5000gm. Sawa sawa na kilo tano Kg 5. Kilo mbili ilikuwa ni rangi ya blue colour A na kilo tatu (3kg) yalikuwa ni rangi ya mkojo, kwa wale wakazi wa Mererani wanajua vizuri wakiona na rangi ya coke ile maji ya kunywa ilikuwa (gm 50). Ndege iliacha aridhi ya Tanzania mnamo saa nne unusu asubuhi, ambako ilichanja mawimbi angani saa mbili na sekunde ya kumi iltua uwanja wa kimataifa Bang kok.Nilifanikiwa kushuka salama nikiwa mtu wa tano. Sikuweza kwenda kwenye soko siku hiyo, nilielekea kwenye maegesho ya gari za kukodi amabako nilikodi gari. “Halo.kutoka hapa hadi Care lodge ni kiasi gani cha pesa?” “Dola tano.Karibu” “Sikuweza kubishana sana kwani niliamini kauli ya ‘nipunguzie bwana’ ni huku kwetu.Alinifungulia mlango wa mbele, nilivuta mguu wangu wa kulia na kuingia ndani mlango wa mbele kulia mwa dereva.Gari hilo lilikuwa ‘Left hand’.Nilienda moja kwa moja kwenye hoteli iliyoitwa CARE LODRGE .Dereva alitumia kama dakika nne kuingia lango la hoteli hiyo.Nilipofika, nilimlipa ujira wake, nikaelekea ofisi za kupokelea wageni(Mapokezi). Sikutaka kwenda kufanya biashara kwa wakati huo. Niliamua kujipumzisha kutokana na uchovu wa safari, jambo la kushangaza nilichokiona mbele ya macho yangu sikuweza kuamini macho yangu kama yalikuwa sawa sawa ama vipi, nilijaribu kupikicha macho pengine ni ule ukungu wa kutokuwahi kupenda. Lakini cha ajabu moyo wangu ulisimama kama sekunde kadhaa, kisha ukaendelea mapigo yake yakawa ya taratibu mno, ambayo sikuweza hata kuyasikia. Nilihisi jasho jepesi likitiririka, kwanza nilijitazama kisha nikamtazama mtu huyo, hata hivyo sikuamini kwamba kwa uzuri wake kamwe ningependwa mtu mweusi tena Mtanzania?. Niliona mwanadada mmoja aliyekuwa amekaa karibu na muhudumu wa mapokezi katika hoteli hiyo, msichana huyo alikuwa Mzungu si mzungu, muhindi si muhindi, mwarabu si mwarabu hata kwenye weusi hakuwepo. Baada ya dakika tano, nikiwa nimemtumbulia jicho la matamanio, alinisalimia . “Kaka habari yako” “Nzuri, sijui nyie”nilijibu salamu kwa wote,nikiwa bado sijabandua jicho usoni mwake.Sikushughulika na huyu mwingine,macho yangu tayari yalishapata chakula.Nilimtizama hamu haikuniisha nikatabani abaki pale pale macho yangu ya shibe. “Mimi mzima”aliitikia msichana huyo na aliyefuata ni wamapokezi. “Hata mimi mzima pia” walinisalimia. Sikupenda kukaa na ule mzigo wenye thamani kubwa niliandikisha jina langu na kuchukua chumba namba kumi.Kila nilipotaka kuondoka kuelekea chumba nilicholipia ,nilisita na kubakia mdomo wazi,mwili ulibweteka nikitamani kufahamiana zaidi na mwanadada yule.Niliamua kujilazimiza kuondoka ingawa nafisi ilitukutika,nilipofungua mlango wangu,niligeuka kumtizama yule mlimbwendekama vile nikihakikisha kama atakuwa pale.Nilimuona nae akinitizama. “Mtoto mtoto,Duu!.Tembea uone mengi”Niliongea akilini nikiwa nafungua mlango,katika kuzungusha funguo mlango ukatii sheria ,ukanipa nafasi ya kuingia.Nilihifadhi Breefcase yangu haraka na kufungua mlango kutoka nje.Nilikuwa nimeshikilia funguo,nikajikuta nikiziachia bila kujijua.Yote ni baada ya kumwona yule binti akiwa ametoka chumba kilichokuwa mkabala na changu. “Kumbe chumba nilichochukua kilikuwa karibu na chumba cha Binti yule niliyesalimiana nae muda mfupi tangu nifike pale.”Nilijisemea moyoni kiwa nimeacha mdomo wazi ,nikimtizama ,alikuwa kajifunga taulo nyepesi kabisa.Tayari kwa sasa alikuwa kanipa mgongo,kila alipovuta hatua , makalio yake yalitikisikia kama mawimbi ya maji baharini.Miguu yake minene iliyobeba umbile la wastani lilijivuta kwa madaha.Nilijikuta nikimtizama hadi alipoishia. Kwa kweli nilimpenda na niliamini angenifaa kuwa mwezi wangu na pambo la ndani. Hata hivyo niliumia moyoni je kama akinikubali nitafanya nini kama baba na mama watakuwa wamenipatia mchumba wa kumuoa?.Wazo hilo lilinijia na nikaamua kulitupilia mbali. Lakini ngoja nisiumize kichwa sijui nitakubaliwa au laa! Kwani nitese nafsi yangu? Nilizidi kuwaza wakati namalizia kufunga chumba. Pasipo kutegemea mara nambona tena akiwa kashikilia mafuta ya lotion. Safari hii alikuwa anakuja kwa mbele,niliweza kufaidi kuisawiri sura yake vema, ilioonyesha umahiri wa muumba.Tembe yake ungeweza kudhania kachoka vile,lakini hapana ukweli halisi.Ule ndio mwendo wake halisi,ikafikia hatua nikadhani hakanyagi chini, kwa jinsi alivyotembea utafikiri anaionea aridhi huruma. Nikajikuta moyo ukinipasuka “paaa” nikiwa na mshangaa nae alinitolea tabasamu nono! lililoshamiri usoni mwake.Tena likiwa limeambatana na mwanya mzuri.Nilishikwa na butwaa kama dakika kadhaa, nikajikuta ubongo ukifa ganzi. Tulibaki macho pima, hapo nilijua dhahiri kama kunapimana hivi.Nikajitizama na kumtizama kwa mara ya pili. Mapigo y a moyo yakaanza kupungua.Hata hivyo nilishindwa kuvumilia yote niliyoyaona kwa safari hii. “Samahani dada naweza kujua jina lako”alikuwa kesha nikaribia. “Yaa!. Jina langu ni Jeniffer John” “Sawa . Ahsante unajina zuri. Naitwa Sweedy Kachenje” nilijitambulisha nikilamba midomo yangu kuua aibu flani iliyochomoza kama mshale wa sekunde na kupotea. Tuliongea mengi na Jeniffer nae hakuwa mvivu wa kujibu maswali na chochote nilichomuelezea, niliamini ndoto yangu ilitimia, yule mwanamke niliyempata angeweza kufunika pengo kubwa maishani mwangu. Hata hivyo katika mazungumzo yetu alinitamkia kwa kinywa chake kuwa nae ananipenda sana, kuliko hata mimi ninavyompenda. Ni binti aliyeukonga moyo wangu na kuuteka kila sehemu ya viungo vya mwili wangu, “Kweli subira huvuta heri” niliongea kimya kimya kwenye mtiririko wa mawazo. Jennifer alikuwa ni mchanganyiko wa Mzungu na mwafrika (chotara) na ni msichana aliyetoka Bara la Africa kama mimi, tofauti ni kwamba yeye alitokea Africa ya kusini, na mimi nilitokea Tanzania. Wala hakujali Nchi niliyotoka kuwa ilikuwa ya kimaskini, inamaana alinipenda na umasikini wangu. Tuliongea na kujikuta mawazo yetu yakiwa sawa, kwa kutaka kunionyesha upendo alikubali ombi langu la kutaka anisindikize kuupitisha usiku uliojaa raha za kila aina. Alidiriki kuacha chumba chake na kuja kulala na mimi, nilimgusia suala la ndoa nalo alilikubali alikuwa tayari kubadili uraia kuwa Mtanzania. Lakini kama angekuwa Mtanzania aliyekuwa Afrika ya Kusini umwambie arudi aolewe Tanzania, angeruka hata futi mia. Kwa upande wa mapenzi nilikoga na penzi motomoto, hakuwa mvivu wa kujishughulisha, tulisaidiana kupitisha usiku huo mwanana uliojaa mahaba ya kila aina, si mlimani tulipanda vichochoroni tulipita kwa nia imara ya kumridhisha Jeniffer aliyeonekana mgeni kwenye ulimwengu huo. Asubuhi kulipopambazuka nilimuaga Jennifer na kuelekea soko la madini ya Tanzanite, lililoitwa King Life. Kabla ya kuondoka nilimuachia namba ya simu email address yangu kwa mawasiliano. Na niliamua kufanya hivyo ili kuwahi na kuwaeleza wazazi habari mpya, wasihangaike kunitafutia mchumba kwani nilishampata mrembo. Nilifanikiwa kuuza madini yote kwa bei nzuri na kurudi Tanzania. Nini kitaendelea hapo usikose mtu wangu...............
Posted on: Tue, 01 Oct 2013 20:58:08 +0000

Trending Topics



th-the-gas-topic-10203220738633564">Dear Whirlpool: I must tell you how very unsatisfied with the gas
Friends, Please check out this new book, Thriving in Turbulent
The current stormy weather is a timely reminder about having
The Argentine hit back after comments made by former #Barca
Today I want to articulate about hidden secret inside men’ minds

Recently Viewed Topics




© 2015