NIONAVYO MIMI HUKU NDIKO KWENYE FUTURE YA TAIFA STARS Ligi - TopicsExpress



          

NIONAVYO MIMI HUKU NDIKO KWENYE FUTURE YA TAIFA STARS Ligi daraja la kwanza imeendelea kuchanua katika viwanja mbalimbali nchini ambapo katika uwanja wa CCM Mbozi wenyeji Kimondo wamesherehesha mashabiki wake baada ya kuitafuna Mkamba Rangersya Morogoro mabao 4-0 Katika mchezo huo uliojaa ufundi na mashambulizi ya kasi. ulimalizika kwa wenyeji kuweka kibindoni pointi tatu,huku wageni wakiondoka vichwa chini,Katika michezo mingine majimaji iliutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wakati ambapo Burkina Faso ya Morogoro ilisafiria nyota yaKurugenzi Mufindi kwa kuifungana bao 1-1. Kimondo ambayo katika mchezouliopita ilitoka suluhu ya kutofungana na Burkina Faso ilionyesha dalili zaushindi tangu mchezo kuanza baada ya mashambulizi kadhaa ya kosa kosakuliandama lango la MkambaBao la kwanza la Kimondolilipatikana mnamo dakika ya 32 kupitia kwa Christopher Kasekwa baada yakuunganisha mpira wavuni ulopigwa kwenye adhabu ndogo. Bao la Pili la Kimondo liliwekwawavuni kupitia kwa Charles Hiza mnamodakika ya 39 ambaye aliunganisha wavunimpira uliotokea wingi ya kushoto kwa Christopher Kasekwa.Hadi mapumziko kimondo ilikuwa mbele ya bao 2. kipindi chapili mchezo uliendelea kwa timu ya Mkamba rangers kujaribu bahati yao lakinihali iliendelea kuwa tete kwa upande wao kwani mnamo dakika ya 87 Geofrey Mlawaaliipatia timu ya Kimondo bao la tatu . Bao hilo lilitokana na piganikupige iliyojitokeza langoni mwa Mkamba baada ya shambulizi lililofanywa nasafu ya ushambuliaji ya Kimondo kufuatia gonga baina ya Charles Hiza, GeofreyMlawa na Godfrey Magetha na kupiga hodikwenye lango la Mkamba huku kipa wake Noel Steven Mkachage akionekana kushindwa kumudu kutokana na ufupi Bao la nne liliwekwa wavuni na Bryson Mponzidakika moja baada ya bao la tatu baada ya kuanzisha shambulio lililombambatiza mlinzi wa Mkamba Thabit Kameta na hivyo mpira huo kumfikia mfungaji ambaye alimchambua kipa wa Mkamba na kuhesabu bao hilo. Ingawa bao la tano liliwekwawavuni dakika ya 90 mwamuzi alipiga filimbi kuwa kipa wa mkamba alikuwa amesukumwa na hivyo mchezo kumalizika kwa Kimondo ikitoka na ushindi wa bao 4 –0dhidi ya Mkamba ya Morogoro.
Posted on: Thu, 10 Oct 2013 05:35:39 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015