#NYUMBANININYUMBANI:Taarifa ya Habari #1.WIZARA ya maliasili na - TopicsExpress



          

#NYUMBANININYUMBANI:Taarifa ya Habari #1.WIZARA ya maliasili na utalii inatoa wito kwa wananchi hususani wanaokaa karibu na hifadhi za wanyama pori kutekeleza dhana ya jeshi la polisi ya ulinzi shirikishi kwa kukabiliana na majangiri kwa kutoa taarifa za kina ambazo zitasaidia kuwanasa na kuwafikisha katika vyombo vya sheria. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salam Msemaji wa wizara hiyo Yustina Malya amesema aliye na taarifa za watu wanaojihusisha na ujangiri azitoe kwa afisa wanyama pori aliye karibu yake, makao makuu ya idara ya wanyamapori, TANAPA au kituo cha polisi. Amesema vita dhidi ya ujangiri ni ngumu hasa ukizingatia kuwa baadhi ya watanzania wanaamini kuwa jukumu la ulinzi ni la serikali pekee dhana ambayo ni potofu kwani uzuiaji hauwezi kufanikiwa kama wananchi na wadau wengine wataendelea kuwa watazamaji tu. #2.WAZIRI wa habari, vijana, utamaduni na michezo Dk. Fenella Mkangara anatarajiwa kufungua mkutano wa siku mbili wa Maafisa wa vijana wote nchini utakaofanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa siku mbili ambao unaanza leo utahusisha watendaji wa mambo ya vijana na maafisa wa vijana wote nchini kuanzia ngazi ya wilaya ambao utakuwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kusimamia na kuratibu maendeleo ya vijana. #3.HABARI ZA KIMATAIFA UMOJA wa Mataifa umesema watu elfu tano wanakufa kila mwezi katika vita vya Syria, ambavyo vimesababisha wingi wa wakimbizi. Maafisa kadhaa wakuu wa Umoja wa Mataifa wamelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililogawanyika kuchukua hatua thabiti za kukabiliana na mgogoro huo uliodumu miaka miwili. Kamishna wa Umoja wa Mataifa anayesimamia masuala ya wakimbizi Antonio Guteress amesema zaidi ya watu milioni 1.8 sasa wamejisajili na Umoja wa Mataifa katika nchi jirani na Syria na zaidi ya watu 6,000 wanaikimbia nchi hiyo kila siku. #4.MJUMBE maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Guinea Bissau, Jose Ramos-Horta, amesema katibu mkuu wa Umoja huo Ban Ki-moon huenda atafanya ziara nchini humo kama uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Novemba 24 utafanyika kwa amani. Ramos-Horta amesema, Ban Ki-moon ameahidi kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo ambaye atachaguliwa kwa njia ya kidemokrasia. Pia Ban Ki-moon atakuwa mwenyekiti mwenza wa mkutano wa wafadhili ambao lengo la mkutano huo ni kukusanya fedha zinazohitajika kufufua uchumi wa Guinea-Bissau. #5.KATIKA MICHEZO UONGOZI wa klabu ya simba umethibitisha kuwepo kwa mchezo wa kimaifa wa kirafiki kati ya timu hiyo na timu ya mamlaka ya mapato ya Uganda URA. Kwa mujibu wa Afisa habari wa klabu ya samba Ezekiel Kamwaga amesema kikosi chao kinatarajia kuwasili jijini Dar es salaam kesho kikitokea kanda ya ziwa kilipokuwa kikifanya ziara ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi uliopangwa kuanza mwezi ujao. Wakati huo huo mratibu wa mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki kati ya timu ya Simba dhidi ya URA kutoka nchini Uganda George Wakuganda amesema maandalizi ya mchezo huo yameshakamilika kwa asilimia 80.
Posted on: Wed, 17 Jul 2013 17:14:28 +0000

Trending Topics



ft:0px; min-height:30px;"> World Premiere: CARBON - Narrated By Leonardo DiCaprio Narrated

Recently Viewed Topics




© 2015