Nakiri baba makosa yangu,naiona wazi dhabi yangu.Nimekukosea wewe - TopicsExpress



          

Nakiri baba makosa yangu,naiona wazi dhabi yangu.Nimekukosea wewe peke yako,Bwana uliye mtakatifu sana.kwa mawazo yangu maneno na vitendo na kwa mutotimiza wajibu.Nimeyatenda mabaya mbele zako,usinihukumu kwa hasira. Uamuzi wako baba ni wa haki,na hukumu isiyolawama. Mimi ni mkosefu tangu kuzaliwa pale tumboni mwa mama yangu.Unitakase kwa husopo yako niwe mweupe kama theluji,baba nijaze furaha na shangwe,nifurahishe tena Rabii. Nihurumie ee Bwana Mungu kulingana na fadhili zako,yafutilie makosa yangu kwa wingi wa huruma zako.Nioshe Bwana hatia yangu.unisafishe dhambi zangu. Baraka zangu zilizoniponyoka,baada ya kugumbikwa na dhabi,ninakusihi kwa unyenyekevu nirejeshee nakuomba.Damu ya mwanao Masiha Yesu Kristo ilomwagika msalabani,ilinilipia deni langu lote,Aliposema yote yamekwisha. Mungu wa haki ninakuomba,usinitupe mbali nawe.Usiniondolee Roho wako,Ee Roho mtakatifu niokoe.Nami ntaimba kwa sauti kubwa ELOHINU UMENIOKOA! Na kabla jua halijatua.Wakosefu watakurejea. Ee Bwana nihurumie...
Posted on: Thu, 21 Nov 2013 04:40:42 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015