Ni vigumu sana kuweza kuamini ila imemtokea jamaa yangu…, - TopicsExpress



          

Ni vigumu sana kuweza kuamini ila imemtokea jamaa yangu…, Nakumbuka kipindi jamaa yupo mwaka wa tatu alijitolea kuwa kampeni meneja wa mwanachuo mwenzake aliyekuwa anagombea nafasi ya urais chuoni hapa…. Kutokana na kipaji alichojaaliwa cha kupendwa na kila mwanafunzi hivyo popote alipo simama watu wengi walijitokeza kumsikiliza, mara nyingi alikuwa anatumia sanaa yake ipasavyo hivyo wanafunzi hupata burudani iliyoambatana na kampeni ndani yake….. Baada ya kampeni kwisha ndipo nafasi ya uchaguzi inapoingia, wanafunzi tunashiriki kupiga kura na hatimaye mshindi anatangazwa, mshindi ni yule aliyekuwa akipigiwa kampeni na rafiki yangu…. Vifijo na nderemo ndivyo vinavyotawala kila kona ya chuo hiki baada ya vifijo na nderemo ndipo simanzi na huzuni inapotawala mara baada ya rafiki yangu kupanda jukwaani na kutoa shukrani zake kwa ushindi walioupata yeye akiwa kama kampeni meneja…….. Alianza kwa kusema, Nawashukuru ndugu wanafunzi wenzangu kwa kuelewa na kuweza kumpigia kura nyingi sana kiongozi huyu aliye mbele yetu, kwa upande wangu sina shaka nae na ningependa kumpa ujumbe huu kisha aufanyie kazi…. Kisha alimgeukia rais wa chuo, mkuu tumekuchagua ili uwe daraja kati yetu na utawala wa chuo hiki, tumekuchagua ili utuwasilishie matatizo yetu panapo husika na kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo, nitaonekana nisiye na busara hata kidogo ndani ya chuo hiki kama haya niliyoyaongea hayatotimizwa ndani utawala wako……na,…..( Jamaa alisita kidogo kIsha akawageukia wanafunzi)……. Alisema, Ndugu wanafunzi wenzangu amini ya kwamba ndugu yako ni yule ambaye yupo tayari kujitolea kufa kwa ajili ya tatizo lako na siyo kwa ajili ya tatizo lake, mnafiki hujidhihilisha panapotokea tatizo….(wanafu nzi walibaki wameduwaa wasijue jamaa anchomaanisha) … hivi ukitaka kujua kama mimi ni ndugu yako wa dhati ninayestahiki upendo wako wa dhati hapa chuoni na popote utakapo niona ungependa kuona nini kutoka kwangu au labda nikufanyie nini?... (wanafunzi wote walibaki wakiangaliana pasipo kupata jibu)…Jamaa aliuliza hivi ni nani anaye mfahamu XXXX yule msichana mrembo ambaye mara nyingi huwa nipo nae cafeteria na maeneo mengine hapa chuoni? Kila mtu alionesha kumjua msichana huyo anyezungumziwa na jamaa…. Jamaa aliuliza swali linguine ni nani aliyewahi kukiona kitambulisho chake cha chuo au hata mahali anapoishi hapa chuoni?( Kila mmoja hakuwa na jibu japo alifahamika hapo chuoni) Ndugu zangu wanafunzi kitambulisho chako ndicho kinacho kutambulisha uhalali wako wa kuwepo eneo hili la chuo na mahali popote pale huendako ukitaka kujua uhalali wa wewe kuishi eneo husika lazima uwe na kitambulisho cha eneo husika….. Nawashukuru sana ndugu zangu wanafunzi kwa kuwa mlionesha upendo wa dhati kabisa kwangu pale nilipo ondokewa na wazazi wangu na kipindi chote niwapo hapa chuoni ila…. ( Jamaa alisita kidogo kisha machozi yakaanza kumlengalenga kisha akaendelea) kwa sasamimi sina wazazi na mlezi wangu mkubwa ni bibi yangu aliye kijijini na mara nyingi alikuwa akinihusia mjukuu wake nisome kwa bidii ili niweze kumwokoa na umasikini aliokuwa nao, yeye ndiye aliyekuwa akinitumia pesa mara kwa mara ninapokuwa na upungufu wa pesa hapa chuoni ila…..(Jamaa alisita tena kisha machozi yalionekana kumtiririka dhahiri na hapo ndipo wanafunzi wengine nao wakaanza kulia japo hawajui nini kinachomliza jamaa yangu)….. Aliendelea, Yule msichana ambaye mlikuwa mkiniona nae mara kwa mara siyo mwanafunzi wa chuo hiki na wala sio mwanafunzi wa chuo chochote hapa Ethiopia hapa yule alikuwa ni changudoa alifanikiwa kunilaghai na kuniachia zawadi hii ya ugonjwa hatari wa ukimwi ambao leo ndiyo imekuwa zawadi ambayo natoka nayo hapa chuoni..( eneo zima lilizizima kwa vilio akiwemo na muhusika wa stori hii, baada ya kama dakika tano hivi ndipo hali ya utulivu ikatawala eneo lile na jamaa akamaliza kwa kusema..) Ndugu zangu wanafunzi KITAMBULISHO CHAKO NDIO UTAMBULISHO WAKO HAPA CHUONI NA MAHALI POPOTE ULIPO kisha jamaa alikaa chini wa masikitiko makubwa kabisa huku akionesha kujutia kupita kiasi…. MWISHO WA STORI JAMANI EEEE! UKIMWI UPO KAMA HUAMINI HATA STORI HII NAYO HAIJAKUSAIDIA?
Posted on: Mon, 19 Aug 2013 06:46:51 +0000

Trending Topics




© 2015