Nimesoma ujinga fulani mahali kwamba eti mwamuzi mmojawapo - TopicsExpress



          

Nimesoma ujinga fulani mahali kwamba eti mwamuzi mmojawapo anayeheshimika sana nchini Martin Saanya anaweza kufungiwa kwa kuvurunda kuchezesha mechi ya Yanga na Coastal Union! Yameelezwa mengi ya kuungaunga na kuizunguka sababu ya hatua hiyo kama kuwa mbali na mpira ulipokuwepo uwanjani nk lakini ukweli unabaki kuwa penalti ya dakika ya mwisho kwa klabu kubwa ndiyo imekera watu. Ujumbe uliopo kwa waamuzi wetu katika fununu hii kama itatekelezwa ni kwamba ili wawe salama lazima Yanga na Simba ziwe zinashinda na si kushindwa au kwenda sare. Pia ili wawe salama, wawe malaika wasiokosea uwanjani na wakishindwa umalaika huo wakosee dhidi ya timu pinzani za Yanga na Simba tu. Unataka kuniambia nini kimefanya Saanya tu afuatiliwe uwanjani mpaka aonekane hakuwa mara kadhaa karibu ya mpira kati ya waamuzi wa mechi zote 14 zilizokwishapigwa sasa hivi? Naomba Wakili mimi nitangaze kuwatetea bure waamuzi wetu wa soka wanaodhalilishwa sana na wanaoumizwa sana kisaikolojia kwa kusakamwa na kusemwa vibaya wanapokosea wakati kila mdau wa soka hukosea kama viongozi wa vilabu, makocha, wachezaji,viongozi wa TFF, watazamaji nk. Nitasimamia kwa nguvu zote adhabu zitolewe kwa wanaowashutumu hadharani waamuzi kama ilivyo kwingine badala ya kuwaadhibu waamuzi kwa kukosea kwani adhabu hizo huwashushia hadhi mbele ya wachezaji na zinawapotezea kujiamini.
Posted on: Mon, 02 Sep 2013 19:04:28 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015