Nimewaza mambo mengi sana baada ya kumaliza kutengeneza hii Juice, - TopicsExpress



          

Nimewaza mambo mengi sana baada ya kumaliza kutengeneza hii Juice, nilipokuwa nainywa nikagundua ni njema sana! Kadhalika msemo huu ndio ulionifanya niwaze mbali 'KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA' Hivi umewahi kuutafakari huu msemo? Umewahi kuwaza kwa nini KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA? Ni kwa sababu it took Him SIX DAYS (Quality time) to finish His Work in Excellence, Juice hii imenichukua three hours kuitengeneza! MY POINT IS: IT TAKES THE QUALITY TIME TO DO THE BEST THING. * Mara nyingi tumelaumu kumbe hatuna muda wa kufanya vitu katika ubora. * Unalalamika ndoa yako imekaa mkao wa sintofahamu kumbe tatizo ni kwamba hujatoa muda ulio bora kwa ajili ya hiyo ndoa. * Ni mara ngapi mpenzi/mchumba wako ametaka appointment mzungumze juu ya misingi ya mahusiano yenu lakini umekuwa ukikwepa na mwisho wa siku mwenza wako kaamua kula kona halafu sasa unaanza kulia, KISA - Umekataa quality time. * Mwanafunzi mzuri ni yule anayejifunza kwenye mazingira magumu, huyu atatoa muda ulio bora kwa kila fursa iliyo mbele yake. ZABURI 119:67, 71, Inasema: 'Kabla sijateswa mimi nalipotea, Lakini sasa nimelitii neno lako. Ilikuwa vema kwangu kuwa naliteswa, Nipate kujifunza amri zako' TUMIA MUDA ULIO BORA KUPATA KILICHO BORA! Kama umejifunza kitu hapa, basi Comment!
Posted on: Fri, 27 Sep 2013 16:29:17 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015